Tuesday, October 31, 2017

TANZANIA YAWA KINARA KATIKA MAPAMBANO YA UKATILI WATOTO BARANI AFRIKA

Na Humphrey Shao Globu ya Jamii

TANZANIA imetajwa kuwa ni nchi ya kwanza barani afrika katika mapambano dhidi ya ukatili watoto kulinganisha na mataifa mengine.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa shirika la Kimataifa linaloshughulikia haki za watoto, Elimu na Ushauri, Michael Gibbons alipokuwa akitoa mada katika mkutano wa kujadili masuala ya ukatili kwa watoto na Wanawake uliofanyika jijini Dar es Salaam Leo.

Gibbons amesema Tanzania ndio nchi pekee Afrika iliyoweka nguvu kubwa katika mapambano ya ukatili wa mtoto pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya elimu kutokana na sera yake ya Elimu Bure.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa afya jinsia Wanawake na Watoto, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Magreth Mussai amesema Serikali inatumia takribani Bilioni 6.7 kutibu naa kushughulikia matokeo ya ukatili.

“katika kulinda watoto baada ya matukio ukatili kutokea Taifa linatumia Bilioni 6.7 kwa ajili ya kushughulikia Mahakamani, Matibabu na hatua zote anazostaili mtoto na Wanawake baada ya ukatili kutokea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki Elimu nchini John Kalaghe amesema asilimia 52.6% ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto hutokea mashuleni jambo ambali limekuwa likipigiwa kelele na wazazi wengi.

Kalaghe amesema ukatili wa watoto ni moja ya jambo ambalo linasumbua katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na kutaja watoto wa kike na wakiume hapa nchini upitia ukatili wa kupigwa mashuleni kwa asilimia 52.6 %.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki Elimu,John Kalaghe akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia haki za Watoto, Elimu na Ushauri, Michael Gibbons akizungumza katika Mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto na Wanawake , Magreth Mussai akizungumza katika mkutano huo kwa Niaba ya Waziri wa Afya Wanawake jinsia na watoto.
Meneja Maendeleo na utawala wa shirika la kutetea Watoto nchini Uganda , Deogratias Yiga. akizungumza kwenye mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki.
baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki.
baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki.
baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki
wadau walioshiriki katika mkutano wa kujadili Masuala ya haki za Watoto na Wanawake katika ukanda Afrika Mashariki wakiwa katika Picha ya pamoja

No comments: