Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi akizungumza na baadhi ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi kabla ya kuwakabidhi bendera mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (katikati) akimkabidhi bendera mmoja wa vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga toka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Erick Shitindi juu ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na
vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini
Sochi nchini Urusi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.
Na. Eliphace
Marwa
JUMLA ya Vijana 31 wanatarajia kuiwakilisha Tanzania katika tamasha
la dunia la vijana linalotarajia kufanyika Jijini Sochi nchini Urusi kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 22 Oktoba mwaka
huu.
Akizungumza
na ujumbe wa Vijana hao leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhiwa bendera
ya Taifa, Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi alisema tamasha hilo litakuwa na zaidi ya washiriki ishirini
elfu kutoka nchi 150 Duniani kote.
Shitindi aliwapongeza vijana hao kwa fursa ya
kuiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo na kuwaomba kuitumia vyema fursa hiyo
kwa ajili ya kuiwakilisha vema na kutangaza
uzuri wa nchi viongozi kwa mataifa mbalimbali.
“Tamasha
hili litatoa fursa kwenu vijana wa Tanzania na mtakapokuwa huko kuzungumzia
mambo mazuri ya Tanzania na hasa kutangaza uzuri wa nchi yetu kwa vijana wa
mataifa mengine” alisema Shitindi.
Aidha
Shitindi aliwaasa vijana hao kwa kutambua kuwa wanakwenda nchi ya ugenini na
hivyo kuwa makini kwa kuwa watakutana na
watu mbalimbali wenye tabia, maadili na itikadi za mlengo tofauti tofauti za
kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi.
“
Kama mnavyofahamu Tanzania inasifika Duniani kote kuwa ni kisiwa cha amani na
utulivu na ni nchi yenye maadili safi, hivyo tunategemea nanyi mtaenda
kuonyesha nidhamu ya hali ya juu huko ugenini” aliongeza Katibu Mkuu Shitindi.
Shitindi
aliwataka vijana hao kueleza uzuri na mandhari ya vivutio vya utalii vilivyopo
nchini ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Mbuga za Serengeti na bonde la Ngorongoro
ambalo ni moja kati ya maajabu saba ya dunia kuwa vipo na ni mali ya Tanzania
na si vinginevyo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Vijana Bi. Venerose Mtenga kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - ambaye ndiye mkuu
wa msafara huo, alimuahidi Shitindi kuwa vijana hao watakuwa mabalozi wazuri
kwa Tanzania.
“Lengo la tamasha hilo ni kuwakutanisha vijana kutoka
nchi mbalimbali duniani ili kujenga mshikamano, kubadilishana uzoefu
kidiplomasia, na uzoefu katika mbinu mbali mbali za maendeleo katika utandawazi”,
alisema Venerose Mtenga .
No comments:
Post a Comment