Na Agness Francis,Blog ya Jamii
Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amezindua kisima cha maji katika mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Buyuni iliyopo Chanika katika Manispaa hiyo.
Katika mahafali hayo yaliofanyika katika Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amesema kuwa ametoa shukrani kwa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki kwa ushirikiano wao wa kutoa msaada wa kisima cha maji ili kusaidia wanafunzi hao ambao kwa sasa wameondokana na tatizo la maji.
Nae Katibu wa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki Ibrahimu Ibrahim ametoa shukrani za dhati kwa kupata ushirikiano na walimu katika kukamilisha zoezi hilo na pia amewataka wanafunzi hao kutunza vema kisima hicho ambacho kitawasaidia kutunza mazingira na kutatua matatizo mengine madogomadogo.
Vilevile pia Mwalimu mkuu Shule ya Sekondari Buyuni ,Bonifasi Mwalwego ametoa shukrani zake kwa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki kwa ufadhili wa kuwaletea mkombozi wa kisima cha maji ambacho kwa sasa kimeanza kuwasaidia kwa matumizi mbalimbali.
Aidha Mwalimu Mwalwego amesema kuwa ikiwa toka shule hiyo ipate usajiri wake mwaka 2006 sasa ni mahafali nane kufanyika shuleni hapo na ametoa wito kwa wanafunzi kuzingatia elimu hasa kwa wasichana wanaohitimu wale wasikivu pamoja na kuwa na nidhamu pindi wanapokuwa majumbani na kutumia vema elimu waliyoipata.
Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizindua kisima cha maji kilichofadhiliwa na Taasisi ya Time for Help ya Uturuki wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na wageni waalikwa na wafadhili Taasisi ya Time for Help ya Uturuki waliojitokeza kutoa msaada wa kisima cha maji wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam
Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Buyuni, Bonifasi Mwalwego akizunguza na wageni waalikwa wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki, Ibrahimu Ibrahim akizungumza na wageni waalikwa akishukuru walimu kwa ushirikiano wao mapaka kukamilisha zoezi hilo la kisima wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam
Wanafunzi wa vidato mbalimbali wa shule hiyo wakitoa burudani ya kucheza nyimbo tofauti tofauti kwa wageni waalikwa kwaya wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo wakisoma risala kwa mgeni rasmi Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne wa Shule hiyo wakitoa burudani ya kuimba kwaya wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment