Na Globu ya Jamii, Dar es Salaam
Wanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti ili kusaidia kupunguza ongezeko la ugonjwa huo na kutakiwa kuwahi mapema kupima kabla ya tatizo kuwa kubwa kwani saratani inaweza kutibika kwa gharama nafuu kabisa.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu na kusema kuwa vituo vya afya vihakikishe vinatenga siku maalum kila mwezi kwa lengo la wanawake kupatiwa huduma ya upimaji wa saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi na huduma hizi zinatolewa bila malipo ili kuhamasisha upimaji kwa wanawake hapa nchini.
"Wanawake wajitokeze kwa wingi katika kupima ili kujua afya zao na hii itasaidia kupunguza saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi kwa kina mama,kuliko kusubiri tatizo liwe kubwa kwani tatizo likiwa dogo saratani inatibika na kwa gharama ndogo kabisa kuliko kukaa na kusubiri kuwa kubwa ". Amesema
Amesema katika kuboresha huduma hizo serikali imenunua mashine za kisasa kabisa 100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi 173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.
Aidha Waziri ametoa onyo kwa waganga wa kienyeji wanaowarubuni watu kuwa wana uwezo wa kutibu ugonjwa huo kutokana na miti shamba na kuwataka kuachana na hio tabia Mara moja kwani dawa za asili hazitibu saratani ila zinatuliza tu.
" Hakuna dawa ya tiba asili inayotibu saratani waganga wa kienyeji waache tabia ya kuwarubuni wananchi kuwa dawa hizo zinatibu saratani jambo ambalo siyo kweli ila dawa hiyo inapunguza tuu maumivu na kama kuna mtu anaudhibitisho kuwa inatibu alete ifanyiwe uchunguzi ili tubaini kama ni kweli inatibu". Amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile amesema kuwa katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini.
"Ifahamike kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020".Amesema.
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya Utaratibu wa utoaji wa matibabu ya Saratani bure kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile akifatilia kwa makini
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile wakipokea vifaa ivyo vilivyotolewa kwa lengo la kufanya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti kwa wanawake nchini ambapo vifaa ivyo vitasambazwa katika vituo vya afya mbalimbali vitakavyotoa huduma hizo
1 comment:
niligunduliwa na saratani mnamo 2019 na nimekuwa nikitafuta tiba tangu wakati huo. Oktoba mwaka jana nilipokaribia kukata tamaa, nilikutana na chapisho kwenye mtandao ambapo nilinakili barua pepe ya mwanamume anayeitwa dr DAWN inayotoa suluhisho la mitishamba kwa magonjwa. niliwasiliana naye na kupata maelewano naye akanitumia dawa ya mitishamba kupitia united parcel service pamoja na maelekezo ya jinsi ya kuitumia. kwa mshangao wangu mkubwa, nilipona baada ya siku 14 za kutumia dawa kama alivyohakikishiwa na daktari.
Niliamua kushiriki hii kwa sababu najua kuwa kuna watu wengi huko ambao wanahitaji msaada. au umtumie ujumbe kwa WhatsApp.+2349046229159 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
Anaweza pia kuponya magonjwa mengi kama hayo
{1}VVU na UKIMWI
{2}Kisukari
{3}Kifafa
{4} Saratani ya Damu
{5} HPV
{6} ALS
Post a Comment