Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru wananchi waliotoa taarifa zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.
Naibu waziri huyo ametoa tahadhari hiyo leo wakati akizungumza na wakazi wa kata za Mgagao na Kirya zilizopo wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Amesema Serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vipo makini na kuhakikisha usalama wananchi wa eneo.
Amesema Serikali ipo makini na ina macho na masikio ya kutosha na ipo kila mahali na kwamba kama kuna mpango mbaya dhidi ya wananchi waliotoa taarifa hizo hautafanikiwa.
"Jambo limeshapita acheni kutafuta mchawi. Mkae mkijua kwamba Serikali ina mkono mrefu atakayethubutu kutenda mambo ataishia kwenye vyombo vya dola," amesema Ulega.
Ulega amedai kupata taarifa za kuwapo kwa baadhi ya wafugaji kuanza vikao vya kumtafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wanachi wa kata za Mgagao na Kirya juu ya kuwatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru wananchi waliotoa taarifa zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.
Mmoja wa wananchi akitoa kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwasili katika kata Mgagao na Kirya wilaya Mwanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya Mwanga wakiangalia zizi la ng’ombe lilokuwa likihifadhi mifugo iliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni na kukamatwa na Serikali.
Semu ya wananchi wakimsikiza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega leo mkoa wa Kilimanjaro.Picha na Emmanule Massaka,Glob ,jamii Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment