Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo amempigia magoti mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuwasaidia kukarabati shule ya msingi Igeleke kwa kuwa miundo mbinu yake imeharibika na sio rafiki kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Akizungumza na blog bwana Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule hii kwanza toka mwaka 1978 hadi leo shule hiyo haijawahi kufanyiwa ukarabati wa kueleweka hivyo inahitajika kukarabatiwa haraka iwezekanavyo.
“Mwandishi ukiangalia majengo ya shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi hawaingalii kwa jicho la tatu kitu kinachotupa shida sisi viongozi wa eneo hili” alisema Madembo
Madembo alisema kuwa shule nyingi zilizojengwa miaka ya 1978 na kuendelea zinamiundombinu ilichoka hivyo serikali na viongozi wa kisiasa kuanza kuzitafutia mikakati ya kuzikarabati ili kuboresha taaluma kwa watoto wetu kuendana na karne ya sasa.
“Hebu angalia hapo juu hili paa muda wowote kuanzia sasa hili paa la darasa linaweza kuleta maafa kwa wanafunzi lakini viongozi wetu hawaliangalii hili swala ndio maana nimemuaomba huyu mbunge Ritta Kabati kusaidia kuarabati” alisema Madembo
Aidha Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi waliotayari kule maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.
“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo” alisema Madembo
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa anafanyakazi na wenyeviti wote wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kuijenga manispaa na kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Iringa.
“Nimekuwa navikao vya mara kwa mara kwa wenyeviti wa mitaa ya hapa manispaa hivyo wenyeviti wa CHADEMA wamekuwa wa kwanza kuniita kila wakati kusaidia kuleta maendeleo katika maeneo husika ndio maana leo unaniona nipo na mwenyekiti wa CHADEMA kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto za hii shule ya Igeleke” alisema Kabati
Kabati aliwataka viongozi mbalimbali kutafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo wananchi nsio kuangalia vyama vinafanya nini.
“Mimi ni kada wa chama cha mapinduzi lakini nimekuwa nikifanya kazi vizuri na viongozi mbalimbali wa kiasa kwa lengo la kuleta maendeleo tu ndio sababu inayosababishwa wapinzani kuniona mimi bora wakati wa kufanya shughuri za kuleta maendeleo” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa ataendelea kufanya ziara kwenye shule zote zenye matatizo ili kuzisaidia kuyatatua matatizo hayo na leo amefanya ziara katika shule ya msingi Igeleke kwa kuziona changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuzitafutia ufumbuzi.
Naye mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kuzitambua changamoto zinazoikabili shule ya msingi Igeleke iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakiwa katika picha nawanafunzi wa darasa la saba
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua madarasa ambayo miundombinu yake imeharibika.
1 comment:
tabia ya wandishi wa habari kupamba na kuweka lugha kama hizi mara zote ndio wanao chochea vurugu na kufanya watu kukata tamaa na kuto kuwa amini watu kutokana na kauri za kuviziana sasa nina sema sijampigia mtu magoti ila nilizungumza vitu ambavyo chama tawala kilipaswa kufanya bila kujadi itikadi zetu yeyote anaweza kufanya ukarabati wa shule ya IGELEKE BILA MTU KUMPIGIA MWINGINE MAGOTI
Post a Comment