Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha
Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Vijijini ikijihuzuru mbele ya wajumbe muda mchache kabla ya mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati
wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida
Vijijini.
Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati
wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida
Vijijini.
Msimamizi wa uchaguzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.
Na Mathias canal, Singida
Wajumbe
wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida
Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya
uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi
wa ngazi ya mkoa na Taifa.
Mkutano
huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya Ilongelo na kuhudhuruwa na
wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu
wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.
Mwenyekiti
mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni
William Mwang'ima Nyalandu aliyepata kura 440, akifatiwa na FATUMA
Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Alex Mdidi
Lissu aliyepata kura 159.
Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika
alisema kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata
taratibu na kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.
Alisema
kuwa pamoja na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa CCM Wilaya lakini pia
nafasi zingine zilizowaniwa ilikuwa ni pamoja na Nafasi Ya Katibu wa
Siasa na Uenezi Wilaya ambapo Richard Niangusha Kwimba aliibuka mshindi
kwa kupata kura 6, nafasi ya pili ni Khamisi Swalehe Kimu kura 35, Iddi Athumani Monko kura 8 na Swalehe Munkumbu Sungi aliyepata kura 3.
Nyingini
ni nafasi ya mkutano Mkuu wa CCM Taifa waliomba ridhaa katika nafasi
hiyo ni watu 14 ambapo kati yao washindi ni Sabasaba Manase, Zainabu
Abdaleah na Khadija Kisuda Lesso.
Nafasi
ya Halmashauri Kuu ya Wilaya waliogombea ni 27 ambapo kati yao
walioshinda ni Sabasaba Manase, Edward Jared Ihondo, Japhet Ntandu Gham,
Justin Joseph Monko, Mohamed Abdallah Ghamayu, Nkumbi Mohamed Kemi,
Zuena Dunya, Simon Mumbai, Shabani Ally Mang'ola, na Wiliamu Mwang'imba
Nyaland.
Nafasi
ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliomba walikuwa watano lakini
washindi kati yao ni Mchungaji Wilson Mtatuu Ihucha, na Sada Njiku.
Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoa ni Sabasaba Manase, Shaban Mang'old na
Edward Jared Ihonde.
Katibu
huyo wa CCM Mkoa wa Singida Bi Grace Shindika alisema kuwa huu ni
wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya wananchama na
viongozi wote waliochaguliwa ili kuongeza ufanisi na nguvu ya chama
katika Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment