Thursday, October 12, 2017

MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za manispaa ya Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.

Akizungumza mara baada ya kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa amefanya ziara katika shule ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya Kibwabwa na kubaini changamoto nyingi ambazo anaanza kuzitafutia ufumbuzi hivi karibuni.

“Nimejionea mwenyewe changamoto zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo ni kazi yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza kuzitatua changamoto hizo”alisema Kabati

Kabati alisema kuwa atakikisha anazikarabati shule hizo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kama nilivyofanya hapo awali katika shule za msingi za Azimio na Kigonzile ambazo kwa sasa zinaubora kama shule za watu binafsi.“Kwa kweli wadau wamekuwa wakinisaidia kufanikisha swala la kukarabati shule za msingi zilizopo hapa manispaa ya Iringa ili kuhakikisha mazingira ya shule zote yanakuwa bora kama shule za watu binafsi” alisema kabati

Aidha Kabati aliwataka viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa kuzitembelea shule hizo mara kwa mara ili kutatua matatizo haya mapema kwa sababu shule nyingi ni kongwe ndio maana miundombinu imeharibika kwa kiasi kikubwa.

“Viongozi wengi tunashinda sana maofisini kuliko kwenda kuyatembelea maeneo yenye changamoto kama hizi za shule za msingi za manispaa ya Iringa kwasababu ukitembelea maeneo yenye changamoto mara kwa mara inakuwa kazi rahisi kuzitafutia ufumbuzi mapema” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa shule nyingi za msingi manispaa ya Iringa zilijengwa miaka 1980 ndio maana saizi miundombinu imeharibika kutokana na kutokarabatiwa mara kwa mara na kusababisha kuendelea kuharibika kwa kuwa hakuna mikakati ya makusudi ya kukarabati shule hizo.

Kabati aliwaomba wananchi na wadau wa maendeleo kutoa ushirikiano wa kutosha ilikufanikisha azma ya kuzikarabati shule hizo na kuacha kuangalia Itikadi ya vyama vya siasa kwa kuwa maendeleo hayana siasa.Naye mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Kibwabwa Isumael Mlenga alimpongeza mbunge huyo kwa kazi anayoifanya ya kusaidia kukarabati shule za msingi za manispaa ya Iringa ni jukumu kubwa analolifanya kwa wanairinga.

“Ni wabunge wachache wenye moyo kama wa Ritta Kabati hivyo tunapaswa kuendelea kumuunga mkono kwenye kazi anazozifanya kwa maendeleo ya watoto wetu wanaosoma katika shule hizo zinazokarabatiwa na mbunge huyo” alisema Mlenga

Karumerita Mbuta,Zubeiry Mlowela na Romana Lutenga ni wajumbe wa kamati ya shule ya Kibwabwa walimpongeza mbunge huyo kwa ziara zake anazozifanya kuzitambua Changamoto zilizopo mashuleni hasa kwenye shule za msingi hivyo tunaomba ziara zako ziwe na matunda kwa kuboresha miundombinu ya shule ulizotembelea.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika moja ya shule ya msingi akiwa katika ziara ya kutambua changamoto na kuzifanyia kazi ili ziwe na ubora kama shule za watu binafsi na kuongeza ufaulo kwa wanafunzi wanasoma katika shule hizo.
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa darasani na wanafunzi wa shule ya msingi Kibwabwa iliyopo kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya kuzitambua changamoto za shule za msingi.

No comments: