Tuesday, October 17, 2017

MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Hajji Manara 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KIKOSI cha Simba kimeanza kuandamwa na majeruhi baada ya John Bocco na Salim Mbonde kuungana na wachezaji wengine baada ya kuumia katika
mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Jumapili iliyopita  dhidi ya Mtibwa Sugar na kushindwa kuendelea mchezo baada ya kupata majeraha.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Hajji Manara amesema kuwa kwa sasa wachezaji wote wapo katika uangalizi wa daktari wa timu.

Amesema beki wa kati Salim Mbonde ambaye ni tegemeo katika safu ya ulinzi ya Simba atakuwa nje kwa wiki nne baada ya kuumia goti katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa mwishoni mwa wiki iliyopita na atakosa michezo takribani minne  ikiwemo Njombe Mji, Yanga, lakini pia anaweza akakosa mechi nyingine mbili dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Ripoti ya madaktari inasema maumivu yake sio makubwa sana lakini anahitaji kukaa nje kwa ajili ya kutumia dawa lakini kama itakuwa vinginevyo basi tutawataarifu.

Kwa upande wa mshambuliaji wa Simba John Bocco aliyeumia kisigino na kupata maumivu ambayo yatamweka nje kwa siku mbili tatu hali itakayomfanya akose mchezo dhidi ya Njombe Mji Jumamosi October 21, 2017.

Akiendelea kuwataja majeruhi katika kikosi cha Simba, Manara amesema kuwa Said Mohamed ‘Nduda’ amerejea nchini lakini tofauti na maumivu aliyoyapata Zanzibar ambayo yalipelekea apelekwe India kwa ajili ya upasuaji, alikutwa na tatizo jingine ambalo alikuwa nalo kwa muda mrefu, kwa hiyo madaktari wakamfanyia upasuaji ambapo kwa bahati nzuri wamefanikiwa kwa asilimia 100.

Nduda atakaa nje kwa wiki nane tangu siku aliyofanyiwa upasuaji, maana yake tutaanza kuwa na Nduda kwenye kikosi kuanzia mwezi December na  Shomari Kapombe Madaktari wameendelea kusisitiza aendelee kupona taratibu matatizo yake ya nyonga inawezekena yalikuwa makubwa tunaamini muda ambao madaktari wamesema akae nje tuendelee kumpa muda na kumvumilia.

No comments: