Na Mary Gwera, Mahakama-Kigoma
KAIMU
Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi/Mkoa-Kigoma, Mhe. Flora
A. Mtarania amewasihi Wadau wa Haki Jinai wa mkoa huo kushirikiana na
Mahakama ili kumaliza mashauri yote yaliyofunguliwa mwaka huu ifikapo
Desemba mwaka huu.
Mhe.
Mtarania aliyasema hayo mapema mwishoni mwa wiki iliyopita Oktoba 06
katika kikao maalum cha Kusukuma Mashauri ‘Case Flow Management Meeting’
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mahakama hiyo ya Mkoa.
“Mpaka
sasa Mahakama ya Mkoa-Kigoma kuna jumla ya mashauri 24 ambayo bado
hayajatolewa maamuzi ‘pending cases’ huku 16 yakiwa mashauri ya Madai na
nane (8) ya Jinai, na kwa upande wa Mahakama za Wilaya kuna jumla ya
mashauri 103 ambayo bado hayajakamilika huku mashauri 79 yakiwa ya Jinai
na 24 mashauri ya Madai,” alisema Mhe. Mtarania.
Alisema
kuwa kesi hizo ambazo zina wastani wa kati ya miezi mitatu (3) hadi
miezi sita (6) tangu kufunguliwa kwake Mahakamani zimekuwa zikikwama kwa
sababu mbalimbali ambazo ni pamoja na kutopatikana kwa Mashahidi hali
inayopelekea haki kutopatikana kwa wakati, upelelezi kutokamilika kwa
wakati, fedha za Mashahidi kutotosheleza uhitaji na kadhalika.
Aliongeza
kuwa ni vyema Suala ya mchakato wa usikilizwaji wa kesi hadi
ukamilikaji wake lifanyike kwa ushirikiano kati ya Mahakama na Wadau wa
Haki Jinai ili haki ipatikane kwa wakati stahiki.
Aidha;
Mhe.Mtarani alisema kuwa lengo la vikao vya pamoja na Wadau wa Mahakama
ni kujadili namna ya kusukuma mashauri ili yaweze kumalizika kwa
wakati, kupeana mikakati ya kushughulikia mashauri na kuhakikisha kuwa
kila mtu anatimiza wajibu wake katika mchakato mzima wa usikilizaji wa
mashauri.
Mhe.
Mtarania aliendelea kusema kuwa vikao hivi hufanyika kila baada ya
miezi mitatu na hiki ni kikao cha tatu (3) kufanyika kwa mwaka huu, huku
akieleza kuwa kabla ya kikao hiki cha ngazi ya Mkoa kufanyika huwa kuna
vikao vya kusukuma Mashauri ambavyo hufanyika kwa ngazi za Mahakama za
Wilaya ili kuwasilisha mipango yao katika kikao cha Wadau cha Mkoa.
“Kimsingi
kwa hatua tuliyofikia sasa vikao hivi vimesaidia kumaliza mashauri
yaliyokuwa yalikaa muda mrefu Mahakamani kutokana na sababu mbalimbali
zilizosababishwa na Wadau,” alieleza Mhe. Mtarania.
Kikao
kilihudhuriwa na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi ambaye ndiye Mwenyekiti,
Mwanasheria wa Serikali Mfawidhi, Mahakimu Wafawidhi wa Wilaya za Kasulu
na Kibondo, Mkuu wa Takukuru-Mkoa, Afisa Uhamiaji wa Mkoa, Mkuu wa
Upelelezi (RCO), Afisa Ustawi wa Jamii, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili
wa Kujitegemea na Mtendaji wa Mahakama-Kigoma.
Hata
hivyo, Wajumbe wa Kikao hicho waliazimia kufanya kazi kwa kushirikiana
ili ifikapo Desemba 30, kesi ambazo hazijakamilika ziwe zimekamilika.
Mtendaji-Mahakama ya Mkoa Kigoma, Bw. Humphrey Paya (kulia) akichangia jambo katika kikao hicho.
Wajumbe
wakiwa katika kikao hicho (katikati) ni Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama
ya Wilaya-Kasulu, wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Mahakama-Kigoma, Bw.
Humphrey Paya na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Ustawi
wa Jamii, Manispaa ya Kigoma.
Wajumbe wakiwa katika kikao.
Kaimu
Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mhe. Flora
Mtarania akiongoza kikao cha Kusukuma Mashauri ‘Case Flow Management
Meeting’kilichofanyika katika Ukumbi wa Mahakama ya Mkoa Kigoma.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao cha Kusukuma mashauri ya Mahakama-Mkoani Kigoma.
Muonekano
wa sehemu ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kigoma,hata hivyo jengo
hilo ni chakavu hivyo linahitaji ukarabati ili liendelee kukidhi
mazingira ya bora ya kutolea haki kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment