Sunday, October 29, 2017

MAFUNDI WA TANESCO WAWEKA KAMBI MBEZI KWA MALECELA KUREJESHA MIUNDOMBINU ILIYOSOMBWA NA MAFURIKO YA MVUA ZA VULI

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
JUHUDI kubwa zimekuwa zikifanywa na wahandisi na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na mvua za vuli zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo jijini Dar es Salaam na hivyo kusababisha maeneo kadhaa ya jiji kukosa umeme.
Eneo la Mbezi chini ni moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya ambapo kwa uchache nguzo nne zimesombwa na maji na kupelekea nyaya za kuafirisha umeme kukatika.
Leo Oktoba 28, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO bi Leila Muhaji, alifanya ziara kutembelea maeneo hayo yaliyoathirika ili kujionea mwenyewe na hivyo kuwa na majibu sahihi kwa wateja abao wamekuwa wakiulizia juu ya tatizo hilo lakukosa umeme.
Akiwa katika eneo la Mbezi chini eneo la daraja la “Kwa Malecela” ambako nguzo hizo zinakatisha kwenye daraja hilo na kukuta mafundi wakienendelea na kazi ya kusimika nguzo na kufunga nyaya.
Kwa mujibu wa Muhandisi Mkuu wa TANESCO Kinondoni Kaskazini Mhandisi Godlove Mathayo, amesema mafundi wanafanya jitihada kusimika nguzo na kushughulikia tranforma mbili moja iliyoko eneo la Victor5ia na nyingine hapo kwa Malecela, na kazi hiyo ikikamilika basi umeme utarejea usiku huu.
:Kuna baadhi ya transoma zimezingirwa na madimbwi ya maji na tunashindwa kuzifikia kwa sasa na pindi maji yatakapopungua kazi ya kuzirekebisha tranforma hizo tutafanya marejkebisho ili umeme uweze kurejea katika hali yake ya kawaida.
“Amesema baada ya matengenezo hayo yanayoendelea sasa, wakazi ambao wanategemea kupata umeme ni wote wa maeneo ya Kwa Malecela, Victoria na Kawe kwa maana ya eneo la Mbezi Chini.” Alisema.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Uhusioano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba radhi wateja waloathirika kutokana na hitilafu hiyo na kuwasihi kuwa wavumilivu kwani mafundi wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha umeme unarejea katika hali yake ya kawaida.
“Lakini niwaombe tu wananchi watoe taarifa pale wanapoona maeneo yao hayana umeme, watufahamishe ili mafundi wafike kwa haraka na kufanya marekebisho, wanaweza kufanya hivyo kupitia anuani zetu na mitandao ya kijamii ya Shirika.” Alisema.
Miundombinu imeathirika kutokana na mvua hizi za vuli lakini nitoe tahadhari umeme na maji haviendani, wananchi wasisogelee miundombinu ya umeme wanapoona nguzo imelala au waya umelala wasiguse watoe taarifa na mafundi wetu ambao wana vifaa maalum watafika mara moja na kuondoa hatari hiyo. Alifafanua Bi. Leila.



 Winchi ikinyanyua nguzo wakati wa urejeshaji miundombinu ya TANESCO eneo la Kwa Malecela Mbezi chini jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2017.
 Fundi wa TANESCO akiwa amebeba vipuri wakati wa zoezi la kurejesha miundombinu ya umeme iliyoathirika na mafuriko ya mvua za vuli enel la Mbezi chini jijini Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.
 Mhandisi Mkuu wa TANESCO Kinondoni Kaskazini, Mhandisi Godlove Mathayo, (kulia), akimuoneyesha Kaimu Meneja Uhusiano, TANESCO, Bi Leila Muhaji, jinsi kazi inavyoendelea eneo la Mbezi Kwa Maalecela jijini Dar es Salaam Jumamosi Oktoba 28, 29017.
 Fundi wa TANESCO akiwa kazini eneo ambalo miundombinu ya umeme iliathirika huko Mbezi Kwa Malecela leo Oktoba 28, 2017
 Fundi wa TANESCO akiwa kazini eneo ambalo miundombinu ya umeme iliathirika huko Mbezi Kwa Malecela leo Oktoba 28, 2017


No comments: