Monday, October 9, 2017

Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola

Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma, akiashiria uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania  (TBS), Prof. Egid Mubofu na kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa IFC-Banki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Uganda na Sudan Kusini, Dan Kasirye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga(K) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma (Kushoto), akipata maelezo kuhusu bidhaa za sola kutoka kwa Meneja Mkazi wa Kampuni ya Solar Sister, Fatma  Muzo,(katikati), pembeni yake ni ANSILA MAKUPA- BUSINESS DEVELOPMENT ASSOCIATE wakati wa uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam mapema iliyopita
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika hafla ya uzinduzi huo mapema wiki iliyopita jijini Dar es salaam.
wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mapema wiki iliyopita

Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 5 2017 – Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC, leo wametangaza uzinduzi wa kampeni ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa.
Nishati inayotumia nguvu ya jua (Sola) na bidhaa za taa zimekuwa zikihitajika zaidi nchini Tanzania, Nchi ambayo familia nyingi za vijijini zinategemea taa za sola zilizo katika viwango duni na bidhaa zingine za umeme kwaajili ya mwanga. Taa ambazo zinaharibika kwa haraka sana na kuwasababishia wateja na watumiaji kupoteza gharama kubwa, jambo ambalo linapunguza uaminifu wao katika uhalali wa bidhaa za sola.
Kampeni hiyo, iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” ina lengo la kuongeza ufahamu wa watumiaji kuhusu manufaa ya taa za kisasa za sola zenye ubora, ambazo zinasaidia wanajamii kufanya maamuzi yenye uhakika wakati wa manunuzi. Itakuwa inaonyesha aina mbalimbali za taa za sola ambazo zina waranti ambazo zinakidhi viwango vya mwanga ulimwenguni (Lighting Global Quality Standard) kampeni hii vile vile inatoa mbinu za kibunifu za biashara katika nishati ya sola kama vile huduma ya Pay-As-You-Go (PAYGO), huduma ya malipo kwa njia ya simu ambayo inamuwezesha mnunuzi kulipa kidogo kidogo, ambayo inafanya makundi mbalimbali yenye uwezo mdogo kifedha kumudu gharama za bidhaa hizo.
Kampeni ya Lighting Africa inataka kuongeza kasi ya matumizi ya bidhaa zenye kiwango bora na zenye gharama nafuu, na inaweza kuboresha kiwango cha maisha ya wanajamii wa vijijini, ambao mara nyingi hutumia bidhaa za mafuta ya taa ambazo sio za uhakika na zina gharama kubwa kama vyanzo vyao vya mwanga.

Kampeni ya IFC na Banki ya Dunia itatoa elimu katika soko la Tanzania kuhusu ubora wa bidhaa, na kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata thamani bora zaidi ya fedha zao,”  Alisema Mhandisi Edward Ishengoma Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala katika Wizara Wizara ya Nishati na Madini wakati wa ufunguzi rasmi wa kampeni hiyo.
Kampeni ya Lighting Africa’s Tanzania itawafikia watumiaji na wanunuzi kupitia njia mbalimbali za matangazo na shughuli za kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari, maonyesho na kampeni ya nyumba kwa nyumba, kulingana na mahitaji ya kaya na kipato nchini kote.
Kampeni ya Lighting Africa inafanyika katika nchi kumi zilizoko kando kando ya mwa jangwa la Sahara. Mpaka sasa programu hii imesha saidia takribani watu milioni 20.5 kufikia mahitaji yao ya msingi ya umeme. (Mwanga na kuchaji simu zao za mkononi) kwa kuuza zaidi ya bidhaa milioni 13 za sola. Lighting Africa/Tanzania ilianzishwa rasmi Septemba 2016 kwaajili ya kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha masoko ya kibiashara kwaajili ya bidhaa za sola zenye ubora nchini Tanzania, na kuwezesha upatikanaji wa taa nzuri zaidi na za kisasa zinazotumia nishati ya sola na upatikanaji wa suluhisho la nishati nchini.

No comments: