Monday, October 16, 2017

KATIBU WA CCM WILAYA YA UBUNGO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI TAWI LA SINZA" A"

Na Mwandishi wetu wa Globu ya Jamii.

KATIKA kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo  cha hayati Baba  wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Chama Cha Mapinduzi(CCM)  katibu wa chama wilaya ya ubungo,Salum  kali  ameweka jiwe la Msingi kwa ajili ya   ujenzi wa ofisi za chama katika tawi la sinza "A"  

Akihutubia wanachama walio  jitokeza  katika shughuli  hiyo  kali amesema, Baba wa taifa  alitengeneza  heshima kwa  Mtanzania  aheshimu  kwanza  maadili ya taifa lake ndio aweze  kuheshimiwa na watu wengine.

aidha kali amesema kuwa ,  Mwalimu Nyerere  aliamini ndani ya  chama  cha Mapinduzi  CCM ndiko  kunapo patikana  viongozi bora  ambao wana uwezo  wa kufanya  kazi  kwa umakini pasipo  malumbano wala fujo  kama tunavyo  ona kwa wenzetu  wa pembeni.

"Mwalimu Nyerere  aliamini  viongozi wa ccm  pekee ndio wanao weza  kusimamia  amani ya nchi hii na ndio kitu ambacho  mpaka sasa chama cha Mapinduzi  kinaendelea kufanya  kupitia Rais   wa  Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli" amesema Kali. 

katibu kali amesema  Baba wa Taifa   alitengeneza  upendo  huku akidumisha  amani  kubwa , ambapo  mataifa  mengi  walikuwa  wakimtumia Mwalimu  Nyerere  kwa kutafuta  Amani  katika nchi zao  na wengi  kuja  kusoma na kujifunza Tanzania  ili  waweze   kwenda kusaidia  nchi zao,  alitolea mfano moja ya nchi ya Msumbiji  na nyingine  nyingi  ambazo  zilikuja  kujifunza nchini  kwetu.

Aidha ameongeza kuwa  sisi leo tunashindwa  kukumbuka  maadili na misingi ya Baba  wa taifa  aliyo  iweka  akiwa na nia ya  kutuunganisha  watanzania  wawe kitu kimoja,  pia waipende nchi  yao ,  wapende  maendeleo ya taifa  lao ili tusonge mbele.

Pamoja na hayo katibu  kali  alizidi  kusema Baba  wa Taifa  aliamini mno kwenye  uaminifu,  uadilifu na uwajibikaji  huku  akiwatilia  mashaka  wale wote  walio kuwa  wanataka  kwenda  ikulu  kwani alichokua anaamini Baba wa Taifa  kuwa  URAIS  ni utumwa  ila  alishangaa kuona watu  wanagombania  kwenda ikulu. 

Adha katibu kali  alisema  walio  zaliwa  mwaka 1974  watakumbuka  ilikuaje , lakini  watu  wanasahau  sana , sasa ivi  vijana  wa Kitanzania  wanabeza  Taifa  la TANZANIA   linalo  ongozwa na ccm, kwa kusema maisha magumu , huku  vijana hao wakiwa wamekaa na kazi  hawataki kufanya  badala yake wamekuwa wakilala mika kwenye mitandao  kuwa maisha magumu  aliwaomba vijana na kuwasihi kufanya kazi kwani akuna kitu kinacho kuja bule na wasipende  kudanganywa .

Alimalizia kwa kusema  kwa mwendo wa  wa mwenyekiti wake wa chama cha mapinduzi CCM  ambae pia ni Rais   wa Tanzania  ana uhakika  kabisa  mpaka  kufikia  mwaka  2020  upinzani Tanzania  utabaki  kuwa ni  mavumbi  kwani  haoni  kazi zozote ambazo  wabunge wa upinzani  wakifanya  zaidi ya vurugu  na kwamba hata wakifanya   bado wanatekeleza  irani ya chama cha  mapinduzi ccm  alitoa  rai kwa wana ccm wote  kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi Baba wa taifa kwa vitendo
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM)  Salum  Kali akishiriki ujenzi wa ofisi za chama kata ya Sinza A.
 Katibu wa chama akizindua jiwe la msingi la  ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Sinza "A"  Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa jumuia ya wazazi mkoa wa rukwa ndg chollaje nae alishiriki ujenzi huo.

No comments: