Monday, October 16, 2017

JAMII YAASWA KUENDELEA KUWASAIDIA WATOTO WENYE UHITAJI NA WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM)Wilayani Geita Bi,Antonia Charles akikabidhi sababuni pamoja na vifaa vya shule kwa Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto cha Bright light na watoto ambao wanaishi kwenye Kituo hicho wakati wa kikao cha kwanza cha Jumuiya hiyo.
Katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapiduzi wilayani Geita,Bi Mazoea Salum ,Akizungumza na kusisitiza wananchi kujitolea kuwasaidia watoto waishio mazingira magumu.
Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia zoezi la utoaji wa msaada kwa watoto waishio mazingira magumu.
Uongozi wa Jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa Bright light pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho.


PICHA NA JOEL MADUKA.

Jamii Mkoani Geita imetakiwa kujitoa kwa moyo wa kupenda kuendelea kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu na wale ambao ni yatima. Rai hiyo ilitolewa na katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapiduzi wilayani Geita,Bi Mazoea Salum wakati alipokuwa akiwakabidhi vifaa vya shule watoto.

wa kituo cha kulea watoto cha Bright light kwenye kikao cha kwanza cha jumuiya hiyo tangu uchaguzi kufanyika ndani ya chama.

Alisema kuwa ni vyema jamii kwa ujumla kukumbuka kuwasaidia watoto ambao wana uhitaji kwani hata kwenye vitabu vya Mungu vimeendelea kuelekeza kutoa msaada kwa yatima,wajane na wale ambao
hawajiwezi kwani kufanya hivyo ni kumpendaza Mungu.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho ,Methew Daniel ameelezea kuwa pamoja na kuendelea kufanya vizuri kwenye kituo hicho bado wanakabiliwa na matatizo ya jamiii kuendelea kukichukulia kituo hicho kuwa kina wafadhili jambo ambalo ni kinyume na kituo kilivyo.

No comments: