Thursday, October 5, 2017

Homa Ini Bado Waendelea Kuwa Tishio

  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai akisisitiza watu kujitokeza kupima afya ili kuthibiti homa ya ini pamoja na magonjwa mengine.
 Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia kongamano hilo.
 Daktari Bingwa wa Magomjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza katika kongamano jinsi ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
Baadhi ya madaktari, wauguzi wa hospitali hiyo na watumishi wengine wakiwa kwenye kongamano hilo leo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, Priumus Saidia akizungumza kwenye kongamano hilo leo.


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetoa ripoti ya robo mwaka tangu ianze kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini ( Hepatitis B) na kutoa tiba ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir .

Akitoa taathimini hiyo leo jijini Dar es salaam,  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo John Rwegasha amesema  muamko ni mkubwa  ambapo katika kipindi cha robo mwaka , Hospitali ya Taifa Muhimbili imesajili wagonjwa  950 .

Akifanunua amesema  hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi  ya wagonjwa itaongezeka na kufika   1800  .Hata hivyo kati ya hao , wagonjwa 540 ndio wamerudi tena Hospitalini kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa uchunguzi huku wagonjwa wengine wakishindwa kufika kutokana na sababu za mbalimbali hususani za kiuchumi , nakuongeza kwamba waliopo kwenye tiba ni  wagonjwa 40.

‘’Idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafika wagonjwa 1800  lakini pamoja na changamoto hiyo hatuwezi kusimamisha huduma tutaendelea kutoa huduma kwani kwa upande wa dawa tumejidhatiti kwa miaka mitano , wagonjwa  hawa wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi  ili aanze kutumia dawa lakini  si wote wanaohitaji dawa’’ amesema DK. Rwegasha.

Kwa upande wake Dk. Tuzo Lyuu amesema tatizo la ugonjwa huo ni kubwa kwani tafiti ambazo zimefanyika ,  watu wanaoenda kuchangia damu asilimia nane wanatatizo hilo na kusisitiza kuwa tatizo hilo si la Tanzania pekee bali  hata kwa nchi zingine zinazoendelea.Kwa mujibu wa Dk. Lyuu kwa sasa tatizo la Homa ya Ini (Hepatitis B) ni kubwa kuliko Ukimwi .‘’ Hapa MNH watu tunaowaona ni vijana na watu wazima na wanaume ndio wengi ingawa hakuna takwimu halisi’’ amesema Dk. Lyuu.

Ugonjwa wa Homa ya Ini unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis B na maambukizi ya ugonjwa huo yanashabiana na njia ya  maambukizi ya Vrusi vya  Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama, kuchangia sindano au vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.

No comments: