Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea ujumbe wa wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya ya nchini Malawi.
Ujumbe huo umeongozwa na Katibu wa Afya nchini humo , Dk. Dan Namarika umehusisha Madaktari , viongozi pamoja na wataalam mbalimbali kutoka katika Wizara hiyo pamoja na taasisi nyingine za afya .
Akizungumza baada ya kupokea ujumbe huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amesema ujio wa watalaamu hao unatoa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Juliethi Magandi amesema katika mwaka wa Fedha 2016-2017 Hospitali imehudumia wagonjwa wa nje Laki Nne , Thelathini na Sita Elfu na Miatatu Tisini na Nne wakati wagonjwa wa ndani waliohudumiwa ni Hamsini na Tisa Elfu na Miatano Hamsini na Tano.
Akizungumzia lengo la ujio wao , Katibu wa Afya wa nchi hiyo Dk. Dan Namarika amesema wamekuja kujifunza jinsi ambavyo MNH inafanya kazi na kutekeleza mipango yake .
Lengo la serikali ya Malawi na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha inaboresha utoaji wa huduma hususani katika Hospitali za Umma nchini humo.Ujumbe usema kuwa umefurahishwa jinsi Muhimbili inavyotoa huduma za kibingwa na kusomesha wataalamu wa afya nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa mafunzo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka Malawi ambao umetembelea hospitali hiyo LEO ili kujifunza jinsi inavyoboresha huduma za afya. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi, Dk. Dan Namarika.
Ujumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk Julieth Magandi akieleza muundo wa hospitali kwa ujumbe wa Malawi.
Wakurugenzi wa Muhimbili wakiwamo watalaamu wengine wa afya wakimsikiliza Dk Magandi leo.
Ujumbe wa Malawi ikiongozwa na wenyeji wao wakiwa katika Jengo la Watoto leo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Dk Juma Mfinga akitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na idara hiyo.
Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.
No comments:
Post a Comment