Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa
wamejipanga kusubiri sherehe za mahafali ya kumaliza mafunzo ya JKT
kuanza. Mafunzo hayo yalifanyika Kambi ya JKT ya Oljoro mkoani Arusha
kwa kipindi cha wiki sita kuanzia tarehe 24 Julai hadi 04 Septemba
2017.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Dkt. Aziz Mlima ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa mahafali hayo akiwa
katika jukwaa kwa ajili ya kupokea heshima kutoka kikosi cha Vijana cha
Operesheni Viwanda (hakipo pichani) ambacho kimejumuisha watumishi 30
wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Mgeni
Rasmi, Balozi Mlima akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshima
yake na kikosi kilichohitimu mafunzo ya JKT ambacho kilijumuisha
watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje
Mgeni
Rasmi, Balozi Aziz Mlima wakiwa wamesimama pamoja na Mwakilishi wa Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (kulia) na Kamanda wa Kambi ya Oljoro kwa
ajili kuangalia vikosi vikipita mbele yao katika mwendo wa pole na kasi
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa kasi
Mgeni Rasmi akikabidhi zawadi kwa waliofanya vizuri zaidi.
Bi. Khadija Othman akipokea zawadi yake
Bw. Graison Ishengoma akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni Rasmi
AWahitimu wa mafunzo ya JKT kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakila kiapo cha utii
Risala
kwa Mgeni Rasmi. katika risala hiyo waliahidi kuyafanyia kazi mafunzo
yote waliyoyapata watakaporejea katika kituo chao cha kazi. Walijifunza
uzalendo, utii, ustahamilivu, ukakamavu na mengine mengi.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao nao washapitia mafunzo hayo katika
awamu ya kwanza wakiwashuhudia wenzao wakihitimu mafunzo ya JKT katika
awamu ya pili.
Burdani ilikuwepo siku ya mahafali. Hapo bendi ya Jeshi ikitumbwiza.
Onesho la Makamandoo hapo mmoja wao amebeba ndoo za maji kwa kutumia meno yake.
Mkuu wa Kambi ya Oljoro akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkuu wa JKT ili amkaribishe Mgeni Rasmi
Mwakilishi
wa Mkuu wa JKT akimkaribisha Mgeni Rasmi atoe hotuba ya kufunga mafunzo
hayo. Kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi alisisitiza umuhimu wa taasisi
nyingine za umma kuiga Wizara ya Mambo ya Nje kwa kupeleka watumishi wao
ili kupata mafunzo ya JKT ambayo ni muhimu kwa kujenga uzalendo,
nidhamu na umoja.
Mgeni
Rasmi akisoma hotuba yake. Alitoa ushuhuda kuwa watumishi walioshiriki
mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wameonesha umahiri mkubwa katika
kutekeleza majukumu yao na ndio sababu amepeleka kundi lingine katika
awamu ya pili. Aliahidi atawapeleka watumishi wa Wizara yake wenye sifa
ikiwemo ya umri (chini ya miaka 40) hatua kwa hatua hadi
watakapomalizika.
Baadhi
ya wageni waliohudhuria mahafali hayo. Hapo afande anateta na
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Bw. Othman Rashid.
Mkurugenzi wa Utawala katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nigel Msangi akimpongeza Bw. Wambura kwa kuhitimu mafunzo ya JKT.
Tumemaliza salama, shukran kwa Wizara kwa kutuandalia mafunzo haya yenye tija kubwa kwetu.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala; Bi. Ngusekela Nyerere na Mwalimu wa
somo la Uzalendo ambaye alikuwa Msadizi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu
Nyerere.
Furaha tumemaliza mafunzo, Kutoka kushoto ni Felista Rugambwa, Teodos Komba na Rose Mbilinyi.
Wakiwa katika pose baada ya kumaliza mafunzo.
Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi na wahitimu wa JKT.
No comments:
Post a Comment