Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt.
Stephen Nindi (aliyesimama)akitoa maneno ya utangulizi kwa wadau wa
Korido ya Mngeta na ukanda wa Magombela-Selous-Udzungwa wilayani
Kilombero juu ya utafiti uliofanywa na wataalam kutoka Tume hiyo
wakishirikiana na Asasi ya kiraia ya African Wildlife Foundation
uliolenga maeneo ya uhifadhi
wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimira na Bioanuai
katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous, iliyofanyika Wilayani Kilombero.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kilombero (DAS) Mh.Robert Selasela(aliyesimama)
akifungua mkutano huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kilombero uliohusu uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati
miliki za Kimira na Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa
Udzungwa-Mgombela-Selous
Bw. Eugine Cylilo mtaalam
kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akitoa tathimini ya tafiti
iliyofanywa na wataalamu kutoka Tume wakishirikiana na African Wildlife
Foundation(AWF) ambayo ilionesha hali halisi ya usimamizi wa mipango ya Ardhi katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous juu ya,utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi
ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.
Wadau wakimsikiliza Bw. Eugine Cylilo mtaalam
kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akiwasilisha utafiti huo.
Bi. Jane Mkinga Afisa mradi wa jumuiko la maliasili Tanzania akichangia maswala juu ya maliasili
Diwani
wa kata ya Mngeta Mh. Flora Kigawa akitaka kupata ufafanuzi wa
changamoto za kutatua migogoro kati ya vijiji na pia kutaka kufahamu
idadi ya wanawake wangapi wanamiliki ardhi katika wilayani Kilombero.
Diwani wa Kata ya Chita Mh. Chelele John akiuliza maswala mbalimbali yahusuyo Ardhi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi.
Albina Burra akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyoulizwa na wadau
kuhusu utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi
ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.
Bw.
Pastor Magingi Meneja wa Programu wa asasi yakiraia ya African
Wildlife Foundation akieleza namna walivyoshirikiana NLUPC katika
utafiti wa uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za
Kimira na
Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous
Muwezeshaji wa Mkutano huo Bw. Geofrey Siima akiendelea kutoa Muongozo wakati wa warsha hiyo.
Afisa
Miradi kutoka asasi ya Kiraia ya Solidardad Bi. Maria Sengelela akitoa
maelezo ya namna wanavyoshirikiana na NLUPC katika swala zima la
matumizi bora ya Ardhi.
Afisa Sheria wa Tume ya Taifa
ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Bi. Devotha Salukele akijibu Maswala mbali
mbali yahusuyo sheria yaliyoulizwa na wananchi kuhusu Ardhi.
Afisa Ardhi Mteule kutoka Wilaya
Kilombero Bi. Syabumi Mwaipopo akifafanua na kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau
wakati wa mkutano huo.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kilombero Bw. Ludwing Ngakoka akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mh. David Lugazio akitoa neno la Shukurani baada ya Mkutano huo kumalizika.
Wajumbe mbalimbali wakiendelea kufuatilia mkutano huo
Picha ya pamoja
Katika kuhakikisha kuwa kuna mipango na
matumizi bora ya ardhi nchini Tanzania, Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya
Ardhi kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia ya African Wildlife Foundation (AWF)
walifanya utafiti wa uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki
za Kimila na Bioanuai katika korido ya Mngeta na ukanda wa
Udzungwa-Mgombela-Selous Wilayani Kilombero.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha utafiti huo
kwa Madiwani, Watendaji Wilaya, Tarafa na Kata, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi alisema kuwa
Tume ilifanya utafiti katika ushoroba wa Mngeta pamoja na ukanda wa
Udzungwa-Magombela-Selous lengo likiwa ni kuangalia mambo mbalimbali yanayohusu
matumizi bora ya Ardhi, umiliki wa ardhi, uhifadhi ya mazingira na Bioanoai
katika maeneo hayo.
Mkurugenzi Mkuu alidokeza kuwa Wilaya ya
Kilombero ni moja ya Wilaya tajiri katika nchi ya Tanzania ambayo ina ardhi
yenye rotuba kubwa inayofaa kwa kilimo cha aina mbalimbali pamoja na uoto wa
aina mbalimbali “Kuna matumizi ya aina mbalimbali ya ardhi katika Wilaya hii,
tuna wakulima, wawekezaji wakubwa katika kilimo, wawekezaji wakubwa katika
misitu, hifadhi ya wanyama pori, kilomo cha kati na kilimo cha wakulima wadogo
wadogo, wafugaji, wavuvi, wafanya biashara ambao kwa umoja wanatengeneza ubia
mbalimbali katika matumizi ya Ardhi” alisema Dkt. Nindi.
Aliongeza kuwa lengo la utafiti huu ilikuwa
kuangalia wadau mbalimbali katika utumiaji, upangaji na usimamizi wa ardhi
wanatekelezaje, kuangalia changamoto za mipango ya matumizi ya Ardhi, umiliki
wa ardhi,uhifadhi wa mazingira na Bioanoai.
“Tupo hapa kwa ajili ya kuwasilisha utafiti
wetu kwamba namna gani mambo haya yanafanyika shughuli hizi za uhifadhi wa
mazingira na Bioanoai, Shughuli za upangaji na matumizi ya Ardhi, umiliki wa
Adhi pamoja na utekelezaji wake na usimamizi zinavyofanyika katika kanda hizi
mbili” alisema Dkt. Nindi.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, mtaalamu
wa mazingira kutoka Tume bwana Eugen Cyrilo, alibainisha changamoto kadhaa
matumizi ya ardhi, umiliki pamoja na uhifadhi wa mazingira. “Changamoto kubwa
iliyobainika katika utafiti huu, ni utekelezaji wa maipango ya matumizi ya
ardhi. Vijiji vingi tulivyopitia vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi, ila
kwa kuwa hakuna usimamizi wa mipango hiyo kwa ngazi ya vijiji, kunakuwa hakuna
utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi waliojitengea” alieleza bwana
Cyrilo.
Aidha, katika upande wa mazingira, ilibainika
kuwa kumekuwa usimamizi usioridhisha hasa kwenye misitu na vyanzo vya maji kwa
baadhi wanavijiji wenyewe au watu kutoka nje ya vijiji kuvamia na kuweka makazi
kwenye misitu ikiwa pamoja na kukata miti bila utaratibu. “Kwenye baadhi ya
maeneo, kumekuwa na uvamizi wa misitu ambapo hapo awali ilikuwa imetengwa kwa
ajili ya uhifadhi, na sehemu zingine tulikuta wanavijiji wakifanya shughuli
ambazo si rafiki kwa mazingira pembezoni mwa mito, hii ni tishio kubwa katika
utunzaji wa mazingira” alisema bwana Cyrilo.
Akichangia katika matokeo ya utafiti huo,
Meneja wa Programu kutoka AWF bwana Pastor Magingi aliwasihi uongozi wa Wilaya
kuja na suluhisho la kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi ili kufanya kazi nguvu
kubwa inayofanywa na na Tume, Wadau pamoja na Halmashauri yenyewe isipotee
bure.
Hatua hii iliwapelekea Madiwani wa Kata
zilizohusika kwenye utafiti huu kupendekeza kuwapo kwa mtaalamu wa Wilaya
atakayehusika moja moja na kusimamia utekelezakji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Wilaya
ili kutoa ripoti ya mara kwa mara juu ya usimamaizi na utekelezaji wa mipango
ya matumizi ya ardhi ili kuwa endelevu na yenye manufaa kwa wananchi.
Utafiti huo ulihusisha Kata nne za ukanda wa
Udzungwa-Magombera-Selous, ambazo ni Msolwa Stesheni, Mkula, Mang'ula B na
Sanje pia kulikuwa na vijiji nane vya Msolwa Stesheni, Mkula, Sonjo,
Msufini,Katurukila, Kanyenja, Magombera na Sanje. Aidha katika korido ya Mngeta
utafiti huo ulihusisha kata sita za Namawala, Igima, Mbingu, Mngeta, Chita na
Mofu pamoja na Vijiji vya Mofu, Ihenga,
Kisegese, Vigaeni, Makutano, Igima, Mbingu, Njage, Mngeta, Mchombe na
Lukolongo.
No comments:
Post a Comment