Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) limesema linaunga mkono juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya Taifa jambo ambalo litasaidia kuchangia kwa kasi harakati za kimaendeleo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugalize katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini ambapo alisema tokea Serikali ya awamu ya tano iingie madaraka inakaribia kutimiza miaka miwili lakini ndani ya kipindi hicho watanzania wameona mambo mengi makubwa yakifanywa kwa ajili ya kuipa nchi maendeleo.
Alisema moja kati ya mambo makubwa ni suala la kiongozi huyo kupamaba na vita dhidi ya dawa za kulevya,kuondoa watumishi hewa serikalini pamoja na wenye vyeti feki, Vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi,kufufua shirika letu la Ndege(ATC) kwa kununua ndege ambazo hivi sasa watanzania wanajivunia kuwa ni mali yao.
Mwenyekiti huyo alisema pia mambo mengine ni Ujenzi wa Reli ya kisasa, Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), utoaji wa ajira zaidi ya 50,000 kwa vijana wahitimu, Kuimarisha utumishi wenye nidhamu na uwajibikaji serikalini, Kuinua kwa kasi uchumi wa nchi yetu kimataifa, Kuboresha sekta ya afya pamoja na kupunguza bei za madawa ya binadamu nchini na mengine mengi yaliyoleta maendeleo ya nchi yetu
Alisema pamoja na hayo lakini Rais Magufuli alionyesha ujasiri mkubwa kwa kuzuia mchanga wa madini ya dhahabu (Makinikia) na kuunda tume ili ichunguze namna nchi ilivyokuwa inapoteza mapatoambayo ilionyesha jinsi watu walivyoibiwa mapato ya Taifa kwa kipindi kirefu.
“Lakini hakuishia hapo Juzi Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Madini ya Almas na Tanzanite iliyochunguzwa na kamati mbili zilizoundwa na Mhe. Spika Jobu Ndugai ripoti ambayo imeonyesha jinsi watanzania tulivyoibiwa kwa kipindi kirefu, Mhe. Rais hakusita kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kupelekea Taifa kupoteza mapato”Alisema
Alisema sambamba na hayo suala la ukamataji wa madini ya Almas kwenye uwanja wa Ndege yaliyokua yameripotiwa kuwa na thamani ya 31.4bn tofauti na uhalisia wake ambapo kitaalamu almas ile ina thamani ya 64bn hii ni hatua kubwa sana ya kiukombozi wa nchi yetu ambayo iligeuka kuwa shamba la bibi kila mtu anajifanyia anavyotaka wazungu wanatuibia wanapeleka mali zetu kwao huku wakituachia mashimo makubwa bila kunufaika na rasilimali zetu.
“Kutokana na hayo tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwa ameonyesha uzalendo wa hali ya juu bila kumuonea mtu haya bila kujali cheo cha mtu ameonyesha namna anavyokerwa na vitendo viovu dhidi ya rasilimali za Taifa na pia kaonyesha uchungu mkubwa wa kuzijali rasilimali za Taifa letu kwa vitendo huku akituonyesha mfano unaopaswa kuigwa na kila Mtanzania katika vita hii kubwa ya kuzilinda”Alisema na kuongeza kila mtanzania anapaswa kuwa mlinzi wa rasilimali hizo kwenye mahali alipo.
Alisema watanzania wamefika hapa walipo kwa sababu ya baadhi ya watu waliopewa dhamana na serikali katika nyadhifa mbalimbali kukosa maadili ya uongozi kwa makusudi ama kwa bahati mbaya (uzembe) ambao umeligharimu Taifa lna kulisababishia kupoteza fedha nyingi ambazo zingeweza kuisaidia serikali yetu kutuboreshea maisha yetu, upatikanaji wa Maji, ujenzi wa barabara, Utoaji elimu bure hadi Chuo Kikuu, huduma za afya nk.
“Hata hivyo sisi kama TAHLISO Tunawataka ndugu zetu waliopewa dhamana na serikali hii ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa nyadhifa mbalimbali wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia maadili na miiko ya kazi zao”Alisema
Lakini pia wakitangulize uzalendo wa nchi yetu kwa maslahi ya Taifa letu bila kuangalia maslahi yao binafsi huku wakitambua kuwa wamesomeshwa na kodi za wanachi wa Tanzania ili kuwatumikia Watanzania kwa moyo safi na weredi mkubwa.
Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo wa Tahaliso aliwataka vijana kuacha kukata tamaa tusikate tamaa wala kukatishwa tamaa na mtu kwa haya yaliyofanyika huko nyuma badala yake wajipe moyo na kumuunga mkono Rais wa nchi ambaye amejitolea kwa nia dhati kurudishia Tanzania Mpya itakayokuwa na kasi kubwa ya kiuchumi.
“Lakini pamoja na hayo tusiache kumuombea kwa mungu ili aweze kumlinbda na kumpa afya njema katika kipindi chake cha uongozi kutokana na dhamira ya kipekee aliyokuwa nayo kulinda rasilimaliza za nchi “Alisema.
No comments:
Post a Comment