Mwenyekiti
wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa huo
Mhe.Anthony Mtaka, tuzo ya cheti kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWAMATA
Taifa, ambayo imetolewa kwa Mkuu huyu wa mkoa kama alama ya kutambua
kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha tuzo ya cheti
aliyokabidhiwa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama
alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo
anazozifanya Mkoani humo.
Kutoka
kulia Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo, Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Katibu wa AMAWATA mkoa wa Dar es Salaam,
Bibi. Millensasha Mneo na Afisa Uhusiano wa AWAMATA, Ndg Shushu Joel
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo ya cheti
iliyotolewa kwa Mhe.Mtaka kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za
kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya Viongozi wa AWAMATA na wadau wengine wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya
Mkuu huyo wa Mkoa kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na
Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na
maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akipongezwa na Katibu wa
Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkoa wa Dar es Salaam,
Bibi. Millensasha Mneo mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi
hiyo ngazi ya Taifa kama alama ya kutambua mchango na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Afisa Vijana, Zena Mchujuko(kushoto) naAfisa Habari(kulia)
wote watumishi katika Ofisi yake mara baada kukabidhiwa tuzo ya cheti na
Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya
kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya
Mkoani humo.
Mwenyekiti
wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu(hayupo pichani) kabla ya kumkabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa na
Asasi hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya kutambua mchango wake na kazi
za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo
Katibu
wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkoa wa Dar es
Salaam, Bibi. Millensasha Mneo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu(hayupo pichani) kabla ya kumkabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa na
Asasi hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya kutambua mchango wake na kazi
za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya
Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua
mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Akikabidhi
tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Mwenyekiti wa
AWAMATA Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo amesema Asasi hiyo
imehamasika kutoa tuzo ya cheti kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa sababu ni
mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na namna
mbalimbali za kuzalisha ajira kwa vijana.
Amesema
Mhe.Mtaka ni moja ya viongozi wabunifu sana na kama kiongozi kijana
amekuwa na maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na
Taifa kwa ujumla, ambapo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda katika
Mkoa kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” na
Kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega.
“Mhe.Mtaka
tumeanza kumfuatilia toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya
Hai mpaka na baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, tumekaa
kama asasi tukashawishika kumpa tuzo hii, kwa sababu amekuwa anafanya
kazi ya kizalendo na maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya
kutengeneza ajira; tena kila wilaya kwenye mkoa wake ina kitu cha
kufanya” alisema Golyo.
Akipokea
tuzo hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameishukuru Asasi
ya AWAMATA kwa kutambua mchango wa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na
akabainisha kuwa imeipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa huo
pamoja na wadau wote wanaounga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo
ya Mkoa na wananchi kwa ujumla.
Mtaka
amesema viongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wataendelea kujenga nuru ya matumaini kwa vijana ambao matarajio yao
makubwa ni kuona kuwa wanapata kitu cha kufanya ili waweze kuendesha
maisha yao.
Ameongeza
kuwa miradi mingi inayoendelea ya Kiwanda cha Chaki, kiwanda cha
kusindika maziwa na mingine inayofanywa katika ngazi ya viwanda vidogo
vidogo ilianzishwa kwa sababu, mkoa unataka kujenga utamaduni kwa
wananchi hususani vijana kujua kwamba wanaweza kuthubutu kwa kuanzia
ngazi ya chini.
“
Pale Mkula Busega tulianza na vijana waliokuwa wanatengeneza viatu pair
mbili tumewapa mtaji wa milioni 12 wameongeza uzalishaji na tumeomba
Baraza la uwezeshaji wananchi Kiuchumi watawapa fedha ili wanunue
mashine kubwa, pia tunajipanga kwa kilimo cha umwagiliaji; tunataka kuwa
Mkoa ambao wananchi wake wana kitu cha kufanya na wanakiona kwenye
vitendo badala ya kukiona kwenye hotuba nzuri.”
Katika
hatua nyingine Mtaka amewaambia viongozi wa AWAMATA kuwa, pamoja na
kutoa tuzo kwa viogozi kama walivyofanya kwake wanapaswa pia kuwakosoa
viongozi hususani vijana bila kuwaonea (kuwakosoa katika haki) pale
wanapoona hawafanyi vizuri, hii itawasaidia kuthibitisha dhamira ya
Mhe.Rais ya kuwateua, maana ya kupewa uongozi katika kipindi hiki na
kubeba dhamana kwa vizazi vijavyo.
Wakati
huo huo ametoa wito kwa Viongozi wenzake vijana kutimiza wajibu wao,
kuepuka maneno yanayowasahaulisha walikotoka wanapozungumzia maisha ya
vijana wenzao na kukubali kukosolewa, ili wajengwe kuwa viongozi wazuri
wa leo na vizazi vijavyo; kwa kuwa matarajio ya Rais katika kuwateua ni
kuwa na kizazi endelevu kwenye uongozi wa nchi.
Asasi
ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ni asasi ya Kiraia
inayojishughulisha na uelimishaji wa uzalendo kwa Watanzania na
kufundisha mbinu za kujitegemea ili kuondokana na umaskini pia inatoa
tuzo kwa watu wanaofanya vizuri masuala mbalimbali ya kizalendo na
kuwasaidia wananchi kutoka katika umaskini.
1 comment:
Safi sanaa Mkuu wa Mkoa you deserve it
Post a Comment