Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwaonyesha wajumbe walioshiriki
Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika
Mashariki mpango mkakati wa miaka mitano wa Kamisheni hiyo (kulia)
Mtendaji Mkuu wa Kamisheni Prof. Kenneth Simala na (kushoto) Rais
Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.
Maryam Kidiko na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.
KUANDALIWA
kwa kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya
Afrika Mashariki ni miongoni mwa juhudi za kuendeleza lugha ya Kiswahili
katika ukanda huo na Duniani kwa jumla.
Hayo
ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia
Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kamisheni ya Kiswahili
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika ukumbi wa Hoteli ya Golden
Tulip iliopo Malindi Mjini Zanzibar.
Alisema
kongamano hilo lililowashirikisha wataalamu wa lugha ya Kiswahili wa
nchi wananchama wa Afrika Mashariki lina umuhimu mkubwa katika historia
ya maendeleo ya Kiswahili duniani pamoja na kupanga mikutano na
kubadilishana utalaamu .
Hivyo Alieleza kuwa ni muhimu kwa kamisheni kusimamia kwa makini hadhi
ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ikitambuwa kwamba ukanda wa
Afrika Mashariki ni sehemu ya Dunia yenye lugha tofauti.
Samia
alisema uratibu na uendelezaji wa Maendeleo na matumizi ya Kiswahili
utaimarisha mchakato na utengamano wa Jumuiya kwa maendeleo endelevu.
“Utengamano wa Jumuiya sio tukio bali ni mchakato ambao unapaswa
kuendeshwa na watu wenye kuelewa vizuri matumizi endelevu ya Kiswahili
“Alisema Makamo wa Rais.
Hata
hivyo alielezea kuwa mafanikio kamili yanategemea mkabala wa
mawasiliano na ushiriki wa raia wote katika maendeleo endelevu ya
Jumuiya . Alisema Kiswahili ni kiungo muhimu kati ya wana Afrika
Mashariki katika kujenga utambuzi na kubaini changamoto pamoja na fursa
zinazofungamana na maendeleo.
Alitaka
kongamano hilo kuonyesha namna ambavyo Kiswahili kinaweza kufanikisha
utangamano na malengo ya kuimarisha maendeleo ya nchi wanachama Afrika
Mashariki. Waziri Samia alionyesha kkufurahishwa kwake na nchi
wanachama kutenga bajeti kila mwaka kwa lengo la kuimarisha na
kuendeleza shughuli za Kamisheni hiyo.
Nae
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe
alisema baadhi ya Nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambazo zilikuwa
nyuma katika kutumia lugha ya Kiswahili wamepiga hatua na kimeweza
kusaidia katika kuharakisha maendeleo yao.
Aliitaka Kamisheni hiyo kushirikiana na Wadau mbali mbali ili iweze kuleta maendeleo kupitia lugha ya Kiswahili.
Kwa
upande wa Waziri wa Habari Utalii , Utamaduni na Michezo Rashid Ali
Juma alisema Serilkali ya Zanzibar inathamini kuwepo Makao Makuu ya
Kamisheni Zanzibar na ameahidi itaendelea kuunga mkono kutokana na
umuhimu wa lugha hiyo.
Katibu
Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Profesa Kenneth Simala alisema Kamisheni itafanya juhudi ya
kuziunganisha nchi wanachama na asasi za kiraia kukikuza Kiswahili.
Sambamba
na hayo alisema Zanzibar imeweza kutowa mchango mkubwa katika Nchi za
Afrika Mashariki kupitia lugha ya Kiswahili katika kukuza lugha hiyo.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo la siku mbili ni ‘KULETA MABADILIKO KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA KISWAHILI.
No comments:
Post a Comment