MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka
Jiji la Shanghai nchini China na kujadili mambo mbalimbali yamaendeleo
jijini hapa ikiwemo suala la uboreshaji wa kituo cha Mabasi Ubungo.
Ugeni
huo uliambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang ambayo
ndiyo imeingia mkataba na Halmashauri ya jiji kwa ujenzi wa kituo
hicho.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya
kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita alisema kuwa ugeni huo
umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo kituo cha mabasi
ubungo.
Alifafanua
kuwa jiji la Dar es Salaam linakaribia kunza kwa ujenzi wa mradi mkubwa
wa kubadilisha kituo cha mabasi ubungo na kwamba hatua mbalimbli
zimeshakamilika ili kupisha mradai huo.Alisema kuwa mara baada ya
kukamilika kwa mradi huo jumla ya watanzania 20,000 watapata ajira jambo
ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwezesha
vijana kuondokana kwenye makundi ambayo sio salama.
Alisema
kufanikisha kwa mradi huo, utasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha
jijini hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kibiashara.“ Leo
nimekutana na ugeni ambapo kwa kiasi kikubwa mnafahamu ndugu zetu hawa
wamekuwa na urafiki mkubwa katika nchini yetu, tumejadiliana mambo mengi
ambayo yote ni yakuleta maendeleo katika jiji letu.
“
Lakini kubwa zaidi ni kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi Ubungo, ambapo
hivi karibuni tunatarajia kuanza kwa mradi huo, na wananchi pia
watajulisha, nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa jiji linafuata
utaratibu katika kutekeleza mradi huo” alisema Meya Mwita.
“
Fursa hii ni kubwa ambayo tumeipata, watanzania watapata ajira,
mzunguko wa fedha kwenye jiji letu utaongezeka, kama Meya wa jiji hili
nimewakaribisha tufanye kazi pamoja, lengo likiwa nikuweka jiji kwenye
muonekano mzuri” aliongeza.Kwaupande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Linghang Cathy Wang alimpongeza Meya Mwita kutokana na aina ya utendaji
wake wa kazi nakuahidi kuonyesha ushirikiano katika utekelezaji wa mradi
huo.
Alisema
kuwa Meya Mwita ni kiongozi anayefanya kazi kwa bidii na umakini na
kwamba kutokana na jitihada hizo za kulijenga jiji , kampuni yao
itafanya kazi na kumuhakikisha kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
No comments:
Post a Comment