Na Tiganya Vincent
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amefanikiwa kumaliza mgogoro kati ya
waliokuwa wafanyakazi 11 wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun iliyokuwa
ikipanua Uwanja wa Ndege wa Tabora na wamiliki wake juu ya kulipwa madai
ya malipo ya muda wa ziada na mapunjo ya mishahara.
Mgogoro
huo ulimalizika jana mjini Tabora baada ya Wamiliki wa Kampuni hiyo
kukubali na kulipa madeni ya wafanyakazi wake ambapo malipo yalifanyika
mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
Hatua
hiyo ilifikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuamuru kuwang’anywa
Hati za kusafiria za viongozi wake wawili wa Kampuni hiyo na kuzuiwa kwa
vifaa vyake vya ujenzi baada ya kuonekana kuwa anataka kuondoka bila
kulipa malipo ya wafanyakazi hao.
Akizungumza
mara baada ya Kampuni hiyo kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wake Mwanri
alisema kuwa amelizika na kazi iliyofanyika na hivi sasa wanaweza
kuchukua hati zao za kusafiria na wako huru kuondoa vifaa vyao vya
ujenzi kwa sababu wamemalizana na watumishi hao bila kinyongo.
Aliomba
Kampuni hiyo ikipata kazi nyingine isisite kuwapa ajira waliokuwa
wafanyakazi wake licha ya mvutano uliotokea na kuongeza kuwa
kilichotekea ndio mwanzo wa kuboresha mahusiano katika siku za baadaye.
Mwanri
alisema kuwa uungwana waliouonyesha kukabali kukaa pamoja na kumaliza
tofauti zao na waliokuwa wafanyakazi wao umeonyesha ni Kampuni
inayostahili kuendelea kupewa kazi nyingine hapa nchini.
Aliwataka
kutofunga milango kwani inawezekana wapo waliokuwa wafanyakazi wao
ambao walisahaulika na wameshaondoka na pindi watakapokuja na vielelezo
vinavyoonyesha kuwa bado wanadai basi wasaidiwe na walipwe haki zao.
Kwa
upande Meneja Mradi wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun Ercan Kavaic
alisema kuwa hana kinyongo na mfanyakazi yoyote yule na yko tayari
kufanyakazi na mtu yoyote akipata kazi nyingine.
Alisema
kuwa Kampuni yake ilikuwa ikihakikisha kila mtumishi anapofikia ukomo
wa mkataba wake inamwongeza mshahara wa mwezi mmoja zaidi ya ule uliopo
katika mkataba na kumpa cheti cha kutambua mchango wake katika kushiriki
Kampuni yake.
Kavaic
alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa kufanikisha kumalizika kwa
tofauti baina ya Kampuni yake na waliokuwa wafanyakazi wake na kuweza
kufika muafaka wa kulipa fedha nusu ya zile ambazo walikuwa wamesama za
shilingi milioni 20 baada ya uchambuzi walikuta madi ni milioni 10.
Akizungumza
kwa niaba ya wafanyakazi wenzake ambaye ni fundi umeme John Mathew
alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Wilaya ya Tabora kwa
kusimamia hadi haki yao imepatikana na kuonyesha moyo wao wa uzalendo wa
kushughulikia matatizo ya wananchi hata ikibidi kwa nguvu kubwa.
Pia
alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun Bw. Kavaic kwa
kubali kukaa meza moja ambayo ndio iliyolea makubaliano na wao kuweza
kupata haki yao na wao walisema wako tayari kufanyakazi naye endapo
atapewa jukumu jingine la upanuzi wa uwanja wa ndege kama alivyoelekeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment