Na. Benedict Liwenga-WHUSM.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
ametoa pongezi za dhati kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu
Youking kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka katika kudumisha
ushirikiano baina ya Tanzania na China hususani katika nyanja za masuala
ya habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Pongezi
hizo amezitoa hivi karibuni wakati wa hafla ya kumuaga balozi huyo
iliyowakutanisha baadhi ya Viongozi wa Chama cha Ushirikiano wa Rafiki
wa Tanzania na China wakiwemo Waandishi wa habari.
Moja
ya mambo makubwa muhimu yaliyofanyika chini wakati wa kipindi cha
Balozi Lu Youking ni tukio la utiaji saini mwezi Machi mwaka huu ambapo
Serikali ya Tanzania na China zilitiliana saini Mkataba wa Ushirikiano
wa Kiutamaduni wa Miaka mitatu ambao utawapa fursa vijana 200 kutoka
Tanzania kila mmoja kwenda China kwa ajili ya kupata mafunzo katika
nyanja mbalimbali za habari, sanaa na utamaduni.
“Balozi
Lu Youking umetuachia zawadi kubwa sana sisi Wanahabari wa Tanzania,
sasa hivi mimi na wenzangiu Wizarani tunakamilisha utaratibu wa
utekelezaji wa Mkataba huu ili tuanze kuutekeleza mapema iwezekenavyo”,
alisema Dkt. Mwakyembe.
Aliongeza
kuwa, Balozi Lu Youking hivi karibuni ameshirikiana na Balozi wa
Tanzania nchini China, Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki katika kuhakikisha
kwamba Waandishi wa habari 10 kutoka Tanzania wanaondoka mwezi ujao
kuelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika masuala
ya habari.
Kwa
upande wake Balozi Lu Youking alisema kwamba, urafiki kati ya Tanzania
na China umekuwa wa afya na imara zaidi ya nusu karne akikumbushia kuwa,
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake
aliwahi kusema kwamba, Tanzania ina marafiki wengi, lakini China ni
zaidi ndiyo maana Rais wa China, Mhe. Xi Jinping alichagua Tanzania kuwa
kituo chake cha kwanza Afrika wakati wa ziara yake ya kwanza nje ya
nchi tangu kuwa mkuu wa nchi.
Aliongeza
kuwa, kila mwaka zaidi ya Wanafunzi 700 kutoka Tanzania huenda China
kwa ajili ya masomo zaidi na kutokana na hilo, matokeo ya ushirikiano wa
China na Tanzania umekuwa wa manufaa katika maeneo yote ya uchumi wa
Tanzania na maendeleo ya jamii na kwa kila maisha ya Mtanzania.
“Uhusiano
wa China na Tanzania umetoa mwongozo kwa Ushirikiano wa Kusini na
Kusini yaani South-South Cooperation, hivyo kutokana na maendeleo ya
ushirikiano huu katika uwezo wa uzalishaji kati ya China na Tanzania na
mpango wa Ukanda mmoja njia moja, tunaamini ushirikiano huu utakuwa na
matunda zaidi”, alisema Balozi Youking.
Urafiki
baina ya Tanzania na China ulianzishwa na Waasisi Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha
Kikomunisti cha China, Bw. Mao Tse-Tung (Mao Zedong) ambapo uhusiano
baina wa nchi hizi mbili kwa sasa umekuwa kwa kasi na kuleta maendeleo
baina ya pande zote mbili.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe(kulia) akimpongeza Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu
Youking wakati alipowasili kwa ajili ya kushiriki hafla ya kumuaga
balozi huyo iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akiongea na wageni waalikwa pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhulia
hafla ya kumuaga balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking
iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking akiongea na wageni waalikwa
pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhulia hafla ya kuagwa kwake
iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Chama cha Ushirikiano wa Urafiki baina ya Tanzania na China, Dkt.
Salim Ahmed Salim (kushoto) akimpongeza Balozi wa China nchini Tanzania,
Mhe. Lu Youking mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuaga balozi
huyo iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
No comments:
Post a Comment