Thursday, September 28, 2017

DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI

Afisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi Agness Mtei akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ya namna vitambulisho vya Taifa vinavyotengenezwa mara baada ya kuzinduzi zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa.

Na Mathias Canal, Singida.

Zoezi linalotekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi la usajili na utambuzi wa watu wanaoishi katika Wilaya ya Ikungi wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea limezinduliwa rasmi huku wananchi wakihamasishwa kutoa ushirikiano katika zoezi Hilo. 

Zoezi Hilo litatekelezwa katika awamu nne ambapo katika awamu ya kwanza utekelezaji wake utakuwa katika Tarafa ya Ikungi yenye Kata sita kwa wananchi wapatao 45,599, Awamu ya Pili itakuwa Ni Tarafa ya Sepuka yenye Kata Saba na wananchi wakiwa Ni 49,035, Awamu ya Tatu Ni Tarafa ya Ihanja yenye Kata nne huku wananchi wakiwa 54,887 na awamu ya nne itakuwa katika Tarafa ya Mungaa yenye Kata Saba na jumla ya wananchi wapatao 35,311. 

Akizungumza Katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi kwenye uzinduzi wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa zoezi Hilo linalenga kupata taarifa sahihi za watu zitakazotumiwa na mifumo Yote ya serikali na binafsi kubadilishana taarifa kwa lengo la kuboresha Huduma na kuinua hali za watu kutoka kipato Cha chini kwenda Cha Kati. 

Alisema umuhimu wa zoezi Hilo Ni Kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi hususani maeneo ya mipakani, Wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji Mali hususani Biashara, usalama katika miamala ya kibenki pamoja na kuwezesha wananchi kukopeshana kirahisi, Upatikanaji kirahisi wa pembejeo na zana za Kilimo, na Wananchi katika Kaya maskini kutambulika haraka na kupata misaada kupitia TASAF. 

Umuhimu mwingine Ni Upatikanaji wa mikopo ya elimu ya just, Kupunguza ukiritimba katika upatikanaji wa Huduma za Jamii na Kupunguza serikali gharama za kusafirisha daftari la wapinga kura na kuwa na daftari lenye taarifa sahihi za watu na mahali walipo. 

Mhe Mtaturu aliwataka wananchi kutoa taarifa sahihi na kutoa ushirikiano wa karibu kwa viongozi, Wataalamu na wasimamizi wa zoezi Hilo waliokasimishwa jukumu la usajili. 

Alisema kuwa wananchi wote wanapaswa kuwa na viambatanisho muhimu ambavyo Ni Cheti Cha kuzaliwa, Kadi ya kupinga kura, Vyeti vya shule, Pass ya kusafiria (Passport), Leseni ya udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya Mfuko wa hifadhi ya jamii, Nambari ya utambulisho ya mlipa Kodi na Kitambulisho Cha Mzanzibari Mkaazi. 

Alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ameagiza kufanyika kwa zoezi Hilo Bure kote nchini ili wananchi waweze kupata haki yao ya Msingi ya kusajiliwa na kutambulika katika Taifa lao.

Mhe Mtaturu alisisitiza kila mmoja kukemea kwa vitendo viashiria vyote vya Rushwa, ama udanganyifu utakaofanywa na wachache wasioitakia mema Nchi kwa kuzorotesha zoezi Hilo.

Katika kuhakikisha zoezi linafanyika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Kupitia Ofisi ya Wilaya ya Ikungi inakamilisha jukumu lake la kusajili wananchi ambao Ni Raia halali pamoja na uchukuaji wa alama za kibaiolojia katika awamu zote nne.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Katibu wa Cha Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Philiph Elieza akitoa salama za chama kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi. 
Wananchi Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe akitoa salamu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Afisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi Bi Agness Mtei akisoma taarifa ya zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Maafisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi wakiwasalimu wakazi wa kijiji na Kata ya Dung'unyiwakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika. Kulia ni Agness Mtei, Doris Niyukuri na Mary Maputa
Wananchi Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Wananchi Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.

No comments: