Mshtakiwa Yusuph Manji anayekabiliwa na shtaka la matumizi ya dawa za kulevya, akijadili jambo na Wakili wake Hajra Mungula kabla ya kupanda kizimbani kwa ajili ya kuanza kujitetea.
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Daktari bingwa Wa magonjwa ya moyo wa Hospital ya Aga Khan, Prof. Mustapha Bapunia (62), ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, inashangaza, Manji katika umri mdogo alionao anamatatizo sugu ya moyo ambayo yanampasa kujilinda sana.
Dkt, huyo ambaye ni shahidi Wa tatu upande wa utetezi katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Manji amedai hayo leo wakati àkitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.Akiongozwà na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, shahidi Hugo amedai, Manji ana vyuma vinne kwenye moyo ni hatari na kwamba ni lazima ajiangalie sana kwasababu anaweza kufa muda wowote.
Amedai katika umri mdogo alionao Manji kuwa na vyuma vinne kwenye moyo inashangaza sana na kitaalamy anapaswa kujiangalia sana.Amedai Februari mwaka huu Manji alipelekwa hospitalini hapo akiwa anasumbuliwa na maumivu kwenye moyo ambapo kutokana na historia ya ugonjwa iliyotolewa na manji mwenyewe na kwamba aliwahi kuzibuliwa mishipa ya moyo mitatu ilizibuliwa India, Dubai na Marekani lakini pia bado alikuwa akipata maumivu inaonyesha kuwa anatatizo sugu la moyo.
Alidai kuwa hata baada ya kumfanyiwa uchunguzi ilionekana kuna mshipa mwingine ulioziba licha ya ile iliyozibuliwa kuwa wazi lakini walipotaka kumzibua alikataa na kuomba apewe dawa kwasababu familia yake na matibabu yake yapo marekani.
Baada ya vipimo walimshauriwa kutumia dawa za aina nne ambazo ni muhimu sana kwasababu ya umri wake mdogo ili ya kupunguza maumivu makali. Kwani vipimo vinaonyesha Manji ana maumivu sugu ya mgongo na kukosa usingizi ambapo alipewa dawa za kupunguza maumivu (Benzodiazepines)ambazo zinatotewa kwa cheti cha daktari lakini baadae tatizo lilijirudia na kurudishwa tena february 24,2017 saa mbili usiku ambapo majibu ya vipimo vilionyesha kapata mshtuko, wakarekebisha na kumuwekea chuma na kuruhusiwa Machi 14,2017.
"Sisi kwa wagonjwa wa moyo tunatumia Morphine ambayo inasaidia kupunguza maumivu makali na dawa kutoka nje zinaruhusiwa lakini ukiwa na mzigo mkubwa lazima uwe na kibali cha TFDA".Katika utetezi wake Manji alikataa mashtaka ya kutumia dawa za kulevya na kudai kuwa amechafuliwa sana, kwani dawa ambazo zinatajwa kwenye hati ya mashtaka, Morphine na Benzodiazepines ni sehemu ya dawa zake anazotumia na hata siku aliyohojiwa Polisi alikuwa akitumia dawa hizo ana uthibitisho wake.
Aidha aliomba kutoa uthibitisho huo mahakamani kama kielelelezo na kuongeza kuwa Uthibitisho wa dawa hizo ulifika kwa njia ya e-mail na sekretari wake ndio alitoa nakala wakati akiwa Hospital ya muhimbili .
Alidai baada ya sekretari wake Maria kupriti ndio akampatia ndipo wakil wake Hajra kuomba karatasi hiyo ipokelewe kama utambulisho mahakamani hapo.Manji alizitaja aina ya dawa anazotumia kuwa ni Aderall, Vicoean, Bercoced,Xanax na Zyban, ambapo alidai Aderal kwaajili ya kuzuia fikra zisipotee akiwa anafanya kazi.
"Dawa hiyo kwa tanzania inajulikana kama nacotin ambazo anakunjwa kila siku na dawa hizo nazipata za siku 90 nikiwa tanzania na nikiwa marekani napewa za siku 30" alidai.
Amedai polisi walienda kukagua nyumbani kwake pia ambapo walichukua Kompyuta, Viza Card, Credit Card, Bima na saa ambavyo hawajamrudishia hadi leo na kudai alishangaa anakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya lakini Polisi walichukua vitu vingine ambavyo havihusiki.
" Hii kesi inatokana na ugomvi wa kibiashara na niq mchezo mchafu, kwani hakuna asiyejua kama walikuwa anagombania Kampuni ya Tigo"alidai na kuongeza."Kesi hii menisababishia athari kubwa sana, binafsi Nimejiuzulu klabu ya Yanga kwa sababu ya dawa za kulevya na niliandika barua kwa Mkuu wa wilaya ya Temeke kuachia udiwani"alidai.
"Heshima yangu imeshuka hata mbele ya viongozi wakubwa akiwemo Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Raila Odinga ambao wananifahamu, hivyo naona aibu".Aidha Manji alipoulizwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis kwamba anajua dawa za kulevya zinakaa muda gani mwilini alijibu ndio.
Alimuuliza Manji aliomba vibali vya kutumia dawa zake ambazo nchini hazipo na kujibu "Ingekuwa biashara ningeomba, lakini hizi natumia kama dawa hivyo zinakibali na uthibitisho maalum kutoka hospitali niliyopewa".
Pia alidai alishapewa onyo aache kutumia sigara lakini amejiaribu bila mafanikio.Pia shahidi wa nne katika kesi hiyo, Dr Khan aliieleza mahakama kuwa yeye ni daktari wa watoto na familia na amekuwa akimtibu Manji toka akiwa na miaka mitatu na hajawahi kuona kiashiria cha kutumia dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment