Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiongeza na Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing na ujumbe wake katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akizunguza na wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmooja kwa ajili ya kupima afya
Balozi wa Jamhuri ya watu wa China anaemaliza Muda wake nchini amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne.
Mhe Balozi wa China akiwa ameambatana na Maofisa wa Ubalozi huo hapa nchini Ameshangazwa na UBUNIFU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda wa kuwasaidia wananchi wengi wa Mkoa kwa WAKATI MMOJA hususani ni wenye vipato vya Chini ambao idadi kubwa hawawezi kumudu Gharama za matibabu nje ya mifumo rasmi iliyowekwa na Serikali mfano wa Bima ya Afya.
Kutokana na Mkusanyiko huo wa Maelfu ya wananchi Mhe Balozi wa China amesema Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imeamua KUUNGA mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda na kuanzia sasa na kuendelea serikali ya ya Jamhuri ya watu wa China itaungana na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam katika kusaidia zoezi upimaji Afya BURE kwa kufanya yafuatayo :-
1. Serikali ya China italeta Madaktari Bingwa kutoka China ambao wataungana na Madaktari wa Timu maalum ya Mhe Makonda ambao wamekuwa wakitoa huduma za upimaji Afya Bure hivyo Madaktari wa Tanzania wataungana na Madaktari wa China katoka kuendesha huduma ya Utoaji wa Afya Bure Mkoa wa Dar es Salaam.
2. Serikali ya China itatoa vifaa vya kisasa vya UPIMAJI ambazo vitasaidia kuongeza kasi ya upimaji kwa watu wengi zaidi.
3. Serikali ya China ITAGHARAMIA dawa kwa watu wasio na UWEZO wa kumudu Gharama za ununuaji dawa mara baada ya kupimwa na kuandikiwa dawa.
Mhe Balozi wa China amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kumuunga mkono Mhe Makonda hatua ambayo imeishawishi serikali ya China kusaidia katika zoezi hilo zuri lenye Malengo ya kutoa huduma bora za Afya kwa Wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda AMEMSHUKURU balozi wa China kwa Niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukubali kuunga mkono Jitihada za kuboresha Afya za wananchi wake, ambapo amesema wazo hilo la kutoa HUDUMA ZA upimaji bure wa Afya alilianza tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya KINONDONI, na kumuhakikisha balozi huyo kuwa hilo litakuwa zoezi ENDELEVU kwa Mkoa wa Dar es Salaam likiwa na Malengo makubwa matatu ambayo ni :-
1. Kuongeza UELEWA kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa Upimaji wa Afya hata kama hawaumwi.
2. Kuwawezesha wananchi WANYONGE kupata huduma za AWALI za upimaji wa Afya ili kuwasaidia mapema katika hatua za AWALI kugundua matatizo yao.
3. Kubaini magonjwa ambayo husababisha VIFO katika hatua za AWALI.
Mhe Makonda amesema kwa ujumla hatua anazozifanya Katia Sekta ya Afya zinalenga kuunga mkono jitihada na kipaumbele cha Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika masuala ya Afya, na ni kwa sababu hiyo ameamua kuendelea kupambana na changamoto zilizoko kwenye Sekta ya Afya pasipo kusubiria fedha za Bajeti ambazo hata hivyo hazitoshelezi mahitaji halisi ya Afya kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment