Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (katikati) akiongea na
waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba
wa udhamini wa ligi
kuu ya soka ya Vodacom 2017/18 wenye
thamani ya shilingi 325,000,000
uliotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro akiongea na waandishi wa habari (hawamo
pichani) wakati wa hafla hiyo.
Raisi wa Shirikiso la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia
akiishukuru benki ya KCB Tanzania kwa udhamini huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (aliyekaa Kulia) na Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia
(aliyekaa kushoto)
wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya soka
ya Vodacom 2017/18 wenye
thamani ya shilingi 325,000,000 uliotolewa na benki ya
KCB Tanzania kwa TFF.
Pamoja nao wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (aliyesimama
kulia), Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (aliyesimama katikati) na
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (aliyesimama kushoto).
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (Katikati) na Mwenyekiti wa Bodi
ya Benki ya KCB Zuhura Muro (wapili kulia) wakikabidhi mfano wa hundi yenye
thamani ya shilingi 325,000,000 kwa Raisi wa Shirikiso
la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (wapili kushoto), ikiwa ni udhamini kwa
ajili ya ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18. Pamoja nao kwenye picha ni Makamu
wa Raisi wa TFF Michael Wambura (wakwanza Kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF
Wilfred Kidao (wakwanza kushoto).
Benki
ya KCB Tanzania leo imetangaza rasmi udhamini mwenza wa ligi ya soka ya
TFF Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi za kitanzania
325,000,000. Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa rasmi leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Raisi WA TFF
Wallace Karia.
Hafla
hiyo ya makubaliano ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi, Benki ya KCB Tanzania, Bi, Zuhura Muro, Mwenyekiti wa bodi
ya Udhamini TFF, Mhe, Mohammed Abdulaziz, Wakurugenzi wa Bodi ya KCB
Tanzania, Wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania, wawakilishi wa vilabu
vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa udhamini huo upo
ndani ya vipaumbele vya benki kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali
za kijamii ikiwemo michezo. “Sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika
kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa
vijana wengi nchini, hivyo benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiunga na
TFF kukuza mchezo wa mpira wa miguu” alisema Kimario.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhuru Muro alisema kuwa “Benki ya KCB
Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya ligi hii na tunaamini kuwa udhamini
wetu utachangia kuleta hamasa kubwa kwa wapenzi wa mpira wa miguu na
kukuza vipaji vya vijana.” Alieleza kuwa udhamini huo utakuwa chachu ya
maendeleo kwa benki, wateja wake, TFF, wachezaji, mashabiki na wananchi
kwa ujumla.
Rais
wa TFF aliishukuru benki ya KCB kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo
ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2017/18. Pia
alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa
michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi
kuu.
No comments:
Post a Comment