Wednesday, September 13, 2017

BancABC yazindua akaunti mpya ya Hundi ya Jiongeze .

 Meneja wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa BancABC,Joyce Malai (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya Hundi ya Jiongeze isiyo na makato yeyote ya mwisho wa mwezi. Kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo Upendo Nkini.
Meneja wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa BancABC,Joyce Malai (kulia) na  Meneja Masoko wa benki hiyo, Upendo Nkini, wakionyesha bango la   uzinduzi wa akauti mpya ya Hundi ya Jiongeze isiyo na makato ya mwisho wa mwezi wakati wa hafla ya kuzindua akaunti hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Lengo ni kufikia Watanzania wengi na waweze kuwa na kaunti za hundi kwa bei nafuu.
Dar es Salaam Tanzania, BancABC imeendelea kuwa Benki inayojiogeza hapa nchini kwa kua wabunifu wa hali ya juu kwenye utoaji huduma zao pamoja na kuboresha huduma hizo za kibenki ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kwa urahisi na hivyo kuwa suluhisho kwenye sekta ya fedha.

Katika kuendelea kudhihirisha ubunifu wa bidhaa zao, BancABC leo imezindua akaunti mpya inayoitwa Jiongeze Hundi akaunti kwa lengo la kupunguza makato ya huduma za uendeshaji akaunti ya mwezi kwa mwezi kwa wateja wote watakaofungua Akaunti ya Jiongeze na Benki hiyo hapa nchini.

Akaunti ya Jiongeze inamfanya mteja aweze kuendesha akaunti ya kibiashara au ya mshahara mara nyingi bila makato ya mwisho wa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja na hivyo kufanya wateja wa BancABC kuweza kufanya miamala mingi ya kibenki kwa Uhuru na urahisi zaidi.

Faida zingine wateja wa Jiongeze akaunti watafurahia ni pamoja na kuangalia salio sehemu yeyote kupitai simu yako ya mkononi, kuweka na kutoa fedha kupitia kwa zaidi ya mawakala 50 ambao wanapatikana sehemu mbali mbali za Dar es Salaam, kupitia mtandaoni na ATM mbali mbali zenye nembo ya visa na pia kupitia applikesheni ya BancABC aliogeza Mrs. Joyce Malai ambaye ni Meneja wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Biashara wa Benki hiyo.

Ikiwa ni benki iliyoshinda tuzo ya kuwa Benki inayokua kwa haraka kwa mwaka 2017, BancABC tunaendelea kuonyesha dhamira yetu ya dhati ya kujiimarisha zaidi kwa kuendelea kuzindua huduma bora na za kibunifu zinazopatikana kwa urahisi na kuendele kufikia Watanzania wengi ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki, aliongeza Mrs. Malai.


"Ubunifu na huduma zetu ndio unafanya BancABC kuwa tofauti kwa hapa Tanzania. Tumeekeleza nguvu katika kukuza na kuongeza matawi yetu ya kibenki ili kila Mtanzania aweze kufikiwa na huduma za kibenki, alisema Mkuu wa Masoko BancABC Mrs. Upendo Nkini huku akitoa wito kwa Watanzania kujitokeza na kutumia hii fursa ya kufungua na kuendesha akaunti ya Jiongeze kwa mwaka mmoja bila makato yeyote ya mwezi.

Aliongeza kuwa BancABC inawakaribisha wafanya biashara na wajasiriamali, kufungua akaunti ya Hundi ya Jiongeze kwakua huduma hiyo itadumu kwa miezi miwili TU.
Benki ya ABC ambayo ni moja ya kampuni tanzu za Atlas Mara, ilishinda tuzo ya kuwa Benki bora inayokuwa hapa nchini Tanzania kwa mwaka 2017 na inatarajia kuzidi kukua hapa nchini kwa kufungua matawi mawili katika mkoa wa Dodoma na Mwanza ndani ya mwaka huu

No comments: