NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema, tayari asilimia 95 ya uboreshaji
miradi ya umeme katika jiji la Dar es Salaam, imekamilika.
Meneja
Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi,
Mahende Mgaya, (pichani juu), amewaambia waandishi wa habari ofisini
kwake jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2017 na kwamba ifikapo
Desemba mwaka huu wa 2017, wananchi na wakazi wa Dar es Salaam wataona
ile hali ya kukatika kwa umeme, mara kwa mara imebadilika.
“Tulikuwa
na jumla ya miradi mipya 18 ya kuboresha vituo vya umeme jijini Dar es
Salaam ili viweze kutoa umeme wa kutosha na wa uhakika, hadi sasa, vituo
vinane vimekamilika kabisa na vinafanya kazi, vimebaki vituo 10 ambavyo
navyo viko katika hatua za mwisho za kukamilika, na ifikapo Desemba,
2017 vituo vyote 18 vitakuwa vinafanya akzi.” Alitoa hakikisho Mhandisi
Mgaya.
Alisema,
kufuatia kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi na idadi ya watu jijini
Dar es Salaam, mahitaji ya nishati ya umeme nayo yameongezeka na hivyo
Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliamua kuchukua
hatua za haraka kuboresha vituo vyake vya umeme ikiwa ni pamoja na
kujenga vipya ili kukidhi mahitaji halisi ya umeme.
“Wafadhili
kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB, World Bank, Finland, na
Japan), walijitokeza na kufadhili miradi hiyo.”Alifafanua.
Kazi
hiyo ya kuboresha vituo hivyo ambavyo ni pamoja na Mbagala, Kurasini,
Kigamboni, Ilala Mchikichini, Kisutu, Mikocheni, Gongolamboto, na maeneo
mengine imekuwa ikifanyika tangu miaka miwili iliyopita lakini kutokana
na matatizo ya hapa na pale, ikiwa ni pamoja na mapingamizi ya wananchi
kuzuia utekelezaji wa miradi hiyo, na wakandarasi, kumepelekea
ucheleweshaji.
Maeneeo
ambayo yamekuwa yakiathirika zaidi na hali hiyo ya kukatika kwa umeme
mara kwa mara ni pamoja na Wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo na baadhi
ya maeneo ya wilaya ya Kinodnoni.
“Nichukue
fursa hii kuwaomba radhi wananchi, hususan wateja wetu, kutokana na
hali hii ya kukatika kwa umeme, lakini napenda pia waelewe kuwa hali
hiyo inatokana na kazi ambayo tumekuwa tukiifanya, na mara nyingi umeme
tunakata siku za weekend, kwa vile shunguli nyingi za kiofisi zinakuwa
zimepungua na hivyo inakuwa fursa nzuri kwetu kufanya kazi.” Alifafanua
Mhandisi Mgaya.
Alisema,
wananchi wanataka umeme, tena ulio bora na wa uhakika, ndio maana
TANSCO imeamua kuchukua hatua madhubuti za kuboresha na kujenga vituo
vipya vya kupoza na kusambaza umeme ikiwa ni pamoja na kujenga lini mpya
za kusafirisha umeme.“Hatu hizi zote lazima ziwe na changamoto za hapa
na pale, lakini kwa kiasi kikubwa TANESCO inaelekea kulitatua tatizo
hilo la umeme jijini Dares Salaam na Mkuranga.”. Alisisitiza.
Wakandarasi na mafundi wa TANESCO wakiwa kazini Moja ya vituo ambavyo vimefungwa mitambo mipya ili kuboresha upatikanaji wa umeme jijini Dar es Salaam. Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kisutu.
No comments:
Post a Comment