Sunday, September 17, 2017

Anna Marrica azindua mradi wa sauti ya vijana MYIDC Temeke

Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica amezindua mradi wa sauti ya vijana katika Halmashauri ya wilaya ya Temeke na kuwataka vijana hao kutokata tamaa katika kutafuta maendeleo ili kujikwamua kiuchumi.

Marrica amesema hayo katika uzinduzi wa mradi uliofanyika kwenye ukumbi wa manisapaa ya Temeke, lengo likiwa ni kutaka kuwapa moyo na kuwapongeza vijana hao kwa hatua nzuri waliofikia katika kuhakikisha wanaleta maendeleo ambapo mradi huo umelenga kuanzia ngazi ya kata ambazo ni Buza, Makangarawe, Kilakala pamoja na Tandika.

Nae Mwenyekiti Mtendaji MYIDC, Ismae Mnikite amesema kuwa lengo pia ni kutaka kuishawishi Halmashauri ya Manispaa hiyo kufanya mchakato wa kutoa taratibu huru za wazi zinazofaa kuwaingiza vijana katika mfumo rasmi wa kutoa maamuzi ikiwemo kushirikisha hatua mbalimbali za uundwaji wa baraza la vijana kunzisha nganzi ya kata na hata hadi kiwilaya kwa mujibu wa tamko la sera ya Taifa ya maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007.

Vile vile Mratibu wa mradi MYIDC, Kissango Mario ametanabaisha kuwa upo umuhimu wa vijana kujengewa uwezo wa kuhamasishwa, utetezi na ushiriki katika maamuzi pamoja na kuandaliwa kimaadili.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri mkuu kazi vijana ajira na wenye ulemavu, Julius Tweneshe amesema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango wa vijana hasa katika swala la kimaendeleo na ametoa ame toa wito kwa vijana wachangamkie fursa mbalimbali zianazojitikeza.
Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica akizungumza na vijana wa mradi wa sauti ya vijana MYIDC na kuwapongeza kwa hatua waliofikia na kuwataka wasikate tamaa katika swala la kutafuta maendeleo. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti Mtendaji MYIDC, Ismae Mnikite akizungumza na vijana wa mradi wa MYID pamoja na kudadafua zaidi lengo la uzinduzi huo ni nikulenga kuanzisha na kuendeleza majukwaa ya vijana kuanzia ngazi ya kata nne 4 ambazo ni Buza, Mkangarawe, Kilakala na Tandika, leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Julius Tweneshe akizungumza na vijana wa mradi wa MYID kwa kutoa wito katika kuchangamkia fursa zinazojitokeza hapa nchini.
Afisa Habari wa chama cha mbio za polepole Manispaa ya Temeke (Jogging) akiuliza swali kwa Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Julius Tweneshe.
Vijana wa Mradi wa sauti ya vijana MYID wakisikiliza kwa makini mazungumzo ya viongozi wakati wauzinduzi wa mradi wa sauti ya vijana MYID uliofanyika katika harmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja wakiwa ni viongozi, vijana wa mradi wa sauti ya vijana MYID, wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari.

No comments: