Tuesday, August 15, 2017

WAZIRI LUKUVI AWATAHADHARISHA WALE WOTE WATAKAOUZA ARDHO KIHOLELA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii , Kilombero

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wananchi kuacha kuuza maeneo yenye hati za kimila na kuwaonya kuwa maeneo hayo yamepimwa na serikali zaidi hawatatozwa kodi kwa wananchi wanaomiliki ardhi za kimila na maofisa arddhi wawatoze kodi wale wenye hati za miaka 99 za umiliki wa mashamba makubwa ya biashara.

Lukuvi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa hatimiliki za kimila zaidi ya 2000 katika Kijiji cha Nyange wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro kupitia Mradi wa Uwezeshaji Umilikishaji Ardhi (LTSP).

Lukuvi amesema hatimiliki hizo zipo kwa lengo la kulinda ardhi ya vijiji husika na kwamba walanguzi wa ardhi hawatapata nafasi kwa kuwa ardhi iliyopimwa haitaweza kununulika kwa mtu ambaye sio wa kijiji hicho. Amesema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya udalali wa ardhi lakini kutokana na ulinzi uliowekwa katika hatimiliki hizo, hawataweza kwa kuwa ardhi haitanunulika.

"Hili ni agizo kutoka kwa Rais Dk John Magufuli kwamba wananchi wote watakaopatiwa hatimiliki za kimila wasitozwe kodi isipokuwa wale wenye mashamba makubwa ya biashara ambao watatozwa kila ekari Sh 1,000. Kwa kuwa hamtalipa kodi, basi fedha hiyo muitumie kuzalisha zaidi kwa manufaa yenu ya baadae," alisema Lukuvi na kuongeza;

"Ardhi iliyopangwa na kupimwa hata kama ardhi ni ndogo inathamani kubwa zaidi ya mtu mwenye eneo kubwa ambalo halina hatimiliki."

Alisisitiza kuwa wananchi waliopewa hatimiliki za kimila wanakopesheka hivyo, benki zote zifungue milango na kuwapatia mikopo stahiki ili kuendeleza mashamba yao na kujiinua kiuchumi. Alieleza kuwa maofisa wa serikali wanapaswa kueleza namna ya kuzalisha mazao mengi kuliko awali na kwamba ardhi isibadilishwe matumizi kama ni ya kilimo au ufugaji itumike kama ilivyotakiwa.

Lukuvi amesema katika miaka ijayo wanatarajia kutoa hati za kimila 300,000 kwa wananchi na kwamba kwa sasa asilimia 20 pekee ya ardhi ndio imepimwa na kupangwa.

LTSP ni mradi wa majaribio wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Mashirika ya maendeleo ya Denmark kupitia Shirika la DANIDA na nchini Sweden kupitia Shirika la SIDA na Uingereza kupitia Shirika la UKaid  ambapo kwa sasa ni katika  Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga mkoani Morogoro. Mradi huo umeanza Julai mwaka jana kwa kazi ya kupima, kubainisha mpango wa matumizi ya ardhi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi ,akizungumza na Wakazi wa Kijiji Cha Nyange Kabla ya kuanza zoezi la Ugawaji hati za Kimila kwa wakzi wa Kijiji Hicho ambao wamepimiwa kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akiwa na Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Masijala ya Kijiji Cha Nyange ambayo itakuwa inatunza kumbukumbu ya hati.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akimkabidhi hati yake Mkazi wa Kijiji Cha Nyange , Bibi Clesencia Namuhoni wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.

Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard akizungumza na wakazi wa kijijii cha nyange juu ya umuhimu wa kumiliki hati za kimila katika kujiendeleza kiuchumi wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.

Mratibu wa Programu, Godfrey Machabe mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.



Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi na Wageni kutoka balozi mbalimbali wakisaini Vitabu vya wageni mara walipowasili katika kijiji cha Nyange Wilaya ya Kilomber



Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.



Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA



Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Morogoro Mch Getrude Rwakare akiuhutubia Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA



Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk .Kebwe Stephene Kebwe, akihutubia Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange katika hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA



Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA








Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Nyange Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Lukuvi na Wadau wa Maendeleo



Wafanyakazi wa mradi wa mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Lukuvi na Wadau wa Maendeleo

No comments: