NA EVELYN MKOKOI – MWABUSALU MEATU
Hatua
kali zitachuliwa kwa wafanyabiashara wanaouza dawa feki za kuuwa wadudu
wa zao la Pamba nchini, Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa
akizungmza na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba katika kata ya
Mwabusalu Wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake jimboni
Kisesa.
Mpina
alisema kuwa wapo wafayabiashara wanaodhoofisha wakulima wa zao la
Pamba kwa kuwauzia madawa yasiyo na nguvu na kutoweza kufanya kazi
kabisa katika zao la Pamba na kupelekea kufa kwa zao hilo na kuwataka
watu hao kuwaletea wakulima dawa bora kabisa na kinyume na hapo wizara
husika itachukua hatua dhidi yao.
Aidha
amewataka wakulima wa kijiji hicho kinacholima zao hilo la mfano
nakutoa mbegu Bora Pekee ya pamba nchini kuacha kilimo cha mazoea na
kutumia fursa hiyo kuangalia kwanza maeneo wanayoishi kutokana na faida
itokanayo na biashara ya zao la pamba kuninunulia chakula cha kutosha na
kutoka kwenye nyumba za tembe na kujenga nyumba za kisasa.
Sambamba
na hilo Mpina amewataka wakulima hao kuzingatia sauala la utunzaji wa
mazingira kwa kuyaandaa mashamba yao kwa wakati huku wakizingatia
changamoto ya mabadiliko ya tabianchi wanayokabilina nayo.
Awali,
Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Pamba cha Geki Investiment
limited na kuutaka uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji mapema
mwakani ili wakulima wa kata ya Mwabusalu waweze kunufaika kutokanana
mauzo ya pamba yao karibu. “Serikali hii inalenga katika kuinua na
kuimarisha uchumi wa viwanda hivyo kiwanda hiki sasa wakati umefika
wakuanza uzalishaji kisikae hapa na kutumika kama ghala kianze kazi mara
moja, vinginevyo hatuta mvumilia muwekezaji huyu kama atashindwa Wizara
husika itafanya kazi yake”. Alisisitiza Mpina.
Serikai
ya awamu ya tano toka iingie madarakani imepandisha bei ya zao la pamba
kutoka bei ya awali ya shilingi 600 kwa kilo mpaka mpaka sh. 1,200
imeelezwa kuwa kata ya Mwabusalu, ni kata ambayo imepata upendeleo kwa
wakulima kuuza Pamba hiyo kwa kiasi cha shilingi 1,320 kwa kilo.
Tafiti
zinaonyesha kuwa kata ya Mwabusalu inalima Pamba ambayo pamoja
namatumizi mengine inatoa Mbegu ambayo inapatika pia katika maeneo
mawili tuu nchini yanii mwabusalu na Ingunga Mkoani Tabora.
katika Picha Roli lililobeba pamba za wakulima tayari kwenda kuuzwa
Naibu Waziri Mpina akingalia ubora wa Pamba ya wakulima katika kijiji cha Mwabusalu leo.
Naibu
Waziri Mpina akipima furushi la Pamba katika Mzani Maalum kabla ya
kuongea na baadhi ya wakulima wa Pamba katika kijiji cha Mwabusalu
jimboni kisesa leo.
Baadhi
ya wakulima wa Pamba wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira (hayupo pichani) alipokuwa akingumzanao katika
kijiji cha Mwabusalu mapema leo.
Picha
ya pamoja ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba
kijijini Mwabusalu, Meatu Mkoani Simiyu leo.
No comments:
Post a Comment