Na Robert Hokororo, Kishapu DC.
Wananchi
wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Afya (CHF) iliyoboreshwa ili wapate
huduma na kuboresha afya zao na hivyo kuweza kushiriki shughuli
mbalimbali za uzalishaji.
Wito
huo ulitolewa jana na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese
wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji shughuli za afya wilayani
hapa.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo katika kijiji cha Malwilo, Mheshimiwa
Nyabaganga Taraba, Kangese aliwataka viongozi wa serikali za vijiji
kuonesha mfano kwa kujiunga na mfuko huo mapema.Kangese
pia aliwataka viongozi hao kuhamasisha kaya zingine zijiunge ifikapo
Oktoba mwaka huu wakiwemo walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF).
Alisema
huduma hiyo ni muhimu kwa wananchi wasiojiweza na wenye kipato cha
chini ambapo kwa sh. 10,000 humuwezesha kuhudumiwa yeye na watu wengine
sita katika kaya kwa mwaka mzima.
Alisema
Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kutengeneza
miundombinu, kutoa vifaa tiba na kuongeza wataalamu wa sekta hiyo ili
waweze kuhudumia wananchi kwa ufanisi.Katibu
Tawala huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi wa CHF iliyoboreshwa
ulianza rasmi Machi 2016 kwa kuimarisha mfumo wa fedha na uoreshaji dawa
na vifaa tiba.
Aidha,
alisema katika wilaya hiyo ni kaya 10,756 zimeandikishwa huku lengo
likiwa ni kaya 42,000 ambapo kila mwananchama anapata kadi na matibabu
mwaka mzima.Aliwataka
watumishi wa afya pamoja na changamoto ya uchache waendelee kuhudumia
wananchi kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo iliyopo wakati
Serikali inaendelea na michakato ya kuongeza wengine.
Kwa
upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya
ya Kishapu, Dk. Josephat Shani aliwataka wajawazito kuhudhuria kliniki
ili kujifungua salama.Alisisitiza
umuhimu kwa wanawake kujifungulia katika hosptali ili kupata huduma
stahiki pamoja na mtoto na kuwa katika hali ya usalama tofaui na
nyumbani.
Dk.
Shani ambaye pia ni mganga mkuu wa wilaya pia aliwataka kufuata
maelekezo ya watoa huduma za afya ili kuepuka kupata matatizo yanayoweza
kutokea wakati wa kujifungua.
Katibu
Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza wakati wa
kampeni ya afya aliyoizindua kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Dk.
Josephat Shani ambaye pia mganga mkuu wa wilaya akizunguza wakati wa
uzinduzi huo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Maguja Daniel akitoa neno wakati wa uzinduzi huo.
Mratibu
wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) mkoa wa Shinyanga, Haruni Kasale
akizungumzia umuhimu kwa wananchi kujiuna na mfuko wa CHF iliyoboreshwa.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Malwilo wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya afya.
Ofisa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wilaya ya Kishapu, Jacob akitoa ufafanuzi kuhusu mradi huo wa CHF.
Katibu
Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza na wananchi
katika kijiji cha Malwilo wakati wa uzinduzi wa kamnpeni hiyo ya afya.
Wananchi wakifuatilia matukio hayo.
No comments:
Post a Comment