Monday, August 7, 2017

WAKANDARASI NCHINI WAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI

Picha ikimuonesha Mkandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende, ambaye anajenga barabara kwa kiwango cha changarawe yenye urefu  wa kilomita 36, eneo la barabara ya mbauda ,Osunyai Mkoani Arusha iko katika hatua za mwisho kukabidhi (Picha na Pamela Mollel)

Wakandarasi nchini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upitaji wamagari makubwa bila ya kuwa na vipimo maalum ambapo hali hiyo imekuwa ikiharibu miundombinu ya barabara ambapo wamekuwa wakitumia gharama kubwa ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kabla ya kukabidhi barabara hizo kwa Serikali.

Hayo yameelezwa leo na mmoja wakandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende am,bae anajenga barabara kwa kiwango cha changalawe yenye ukubwa wa kilomita 36 eneo la barabara ya mbauda ,Osunyai iko katika kiwango cha changarawe ambapo yuko katika hatua za mwisho kukabidhi ambapo iko katika wilaya ya Arusha,Mkoa wa Arusha.

ALiongeza kuwa katika kutekelezaji wa kujenga barabara hizo ,Serikali itaweka utaratibu wa kupima magari hayo itawasaidia kuweza kutunza barabara hizo na kuweza kutotumia gharama kubwa kwa wakandarasi .

Kwani Serikali italazimika kutoa pesa za mara kwa mara kuwalipa wakandarasi kwa ajili ya kufanya marekebisho ambapo hali hiyo inawatia hasara Serikali na kuwa na matumizi mabaya ya pesa hizo.

Hata hivyo ameitaka Serikali kuweza kutenga maeneomaalumu ya kuweza kupatikana kwa madini ya udongo na mchanga ili kuwezwsha wkandarsi kupata madini hayo kwa urahisi kwani hivi sasa wanapata changamoto kubwa katika udongo huo..

Aliongeza kuwa hivi sasa wananunua udongo huo kwa wananchi ambapo wamekuwa wakiwauzia kwa gharama kubwa hali ambayo imekuwa ikiwagharimu pesa nyingi ukilinganisha na hali halisi..

Kwa upande wake meneja wa Tanroad Mkoa wa Arusha Mhandisi John Edward Kalupale alisema kuwa kuhusu suala hilo la upitaji wa magari makubwa katika barabara inayijengwa ya Mbauda Osunyai ambapo alisema kuwa kisheria hawaruhusiwi kuweka mizani kutokana na kuwa na barabara hiyo kutokuwa na lami. ambayo hivi sasa iko kiwango cha changalawe.

Aliongeza kuwa wasafirishaji ni waharibifu lakini wapende nchi yao na kuwa makini katika kutumia barabara zinzoboreshwa kwa viwango vyote kuanzia changarawe mpaka lami kwani maendeleo yoyote yale yanaletwa na uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara zote.

Ambapo katika barabara hiyo ya osunyai mbauda wamekuwa yakipita magari makubwa ambayo yanajaza michanga na udongo kupita kiasi na pia wanachanganya watu na michanga hhiyo hali ambayo imekuwa ikiharibu barabara hiyo badala yake amewataka madereva wawe wazalendo katika kutumia barabara hizo ili kuweza kuleta manufaa zaidi kwa watumiaji wote ili kuweza kuzitunza na kuepusha serikjali kuweza kutumia pesa nyingi katika kujenga barabara hizo.

Mhandisi John alisema kuwa arusha bado kunakabiliwa na changamoto kubwa ya ardhi lakini wanafata taratibu za kuwezesha kupatikana kwa ardhi ilikuweza kuepuka kupata madini udongo pindi wakandarasi hao wanapohitaji kupata malighafi ya kutekeleza miradi wanyopewa na serikali.

Katika kuweza kupata ufumbuzi wakudumu wapo katika hatua za awali ambapo upembuzio yakinifu wa kina unaendelea katika mhandisi mshauri unaendelea.

Ambapo wanatarajia kuweka lami kilomita 400 kuanzia barabara ya Arusha,osunyai .olkesimate mpaka dosidosi Kongwa ili kuweza kumaliza changamoto mbalimbali zilizoko .
Kwa upande wake dereva wa daladala kutoka mbauda mpaka Olkesimati Erasto Msuya alisema kuwa marekebisho hayo ya barabara yasmewarahisishia sana katika kupeleka abiria hao katika maeneo hayo kwa kabla ya marekebisho hayo walikuwa wanapata tabu na changamoto kubwa sana katika kuweza kutumia na kupelekja abiria eneo hilo.

Anapongeza sana Serikali ya awamu ya tano katika kujenga miundombinu ya barabara na kuboresha maeneo ya barabara mbalimbali nchini.

No comments: