Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akitowa shukrani
zake kwa Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar kwa ushirikiano wao
kuwezesha kupa umeme kwa wakati na katika kijiji cha Tunguu Uwandani
Wilaya ya Kati Unguja, wakiwa katika sehemu iliowekwa Transfoma kwa
ajili ya kupokea umeme katika kijiji hicho na kutowa huduma hiyo kwa
wananchi zaidi ya mia moja kupata huduma hiyo.
Meneja
Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO Hassan Ali akitowa maelezo
wakati wa hafla hiyo ya kupokea shukrani zilizotoka kwa Wananchi wa
Jimbo hilo na Mwakilishi wao kwa msaada wao wa usambazaji wa umeme kwa
wakati na kupata fursa ya kupata hudumi hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Tunguu Uwandani akitowa shukrani
za wananchi wa kijiji hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika eneo
lililowekwa transfoma ya kusabaza umeme katika eneo hilo na kutowa
huduma kwa wananchi zaidi ya mia moja.
Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza wakati
wa hafla hiyo ya kutowa shukarani kwa Shirika la Umeme Zanzibar kwa
msaada wao kukamilisha zoezi hilo la usambazaji wa umeme katika Kijiji
cha Tunguu Uwandani Wilaya ya Kati Unguja.hafka hiyo imefanyika katika
kijiji hicho tunguu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Ally Halil Milza
akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuwataka wananchi wa kijiji hicho
kuitumza miundo mbinu hiyo na kuahidi kusambaza umeme kwa wananchi wa
vijiji jirani kwa kuongeza nguzo 16 zilizobakia ili kuweza kupatikana
kwa huduma hiyo kwa wananchi hao.
Baadhi
ya Wananchi wa Kijiji cha Tunguu Uwandani wakiwa katika eneo la hafla
hiyo wakisikiliza nasaha zilizokuwa zikitolewa na wahusika.
Sheha wa Shehia ya Tunguu Uwangani akisoma dua baada ya hafla hiyo kumalizika ya kutowa shukrani
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Ally Halil Mirza
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme
Zanzibar ZECO wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kijiji hicho
baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said akizungumza na
wananchi wa Jimbo lake baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment