BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeridhishwa na idadi kubwa ya watii
kutoka nchini China na kuelezea kuwa endapo kutakuwa na safari za
ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kutasaidia kupunguza gharama
za safari na pia kuchochea utalii.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliwaambia
waandishi wa habari jijini hapa juzi kuwa endapo kutakuwepo na ndege
ya moja kwa moja kutoka Tanzania mpaka China, idadi kubwa ya watilii
kutoka nchi hiyo itaongezeka na pia mataifa mengine, hivyo sekta ya
utalii uchangia zaidi mapato ya serikali.
akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembeza waandishi
waandamizi wa habari kutoka nchini China katika hifadhi za Ngorongoro
Crater na Manyara,Jaji Mihayo alisema vivutio vya utalii vilivyopo
hapa nchini ni tunu kubwa kwa taifa na pia vinawaleta watalii kutoka
sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi(wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja waandishi Waandamizi wa habari kutoka China walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara na kujionea fahari ya Tanzania. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.
“Ujio wa wanahabari hawa ni fursa kwetu kwani watakwenda kuwa mabalozi
wazuri kwa kutoa machapisho na habari nchini kwao juu ya vivutio vya
utalii vilivyopo Tanzania,” alisema na kutoa wito kwa waandishi wa
ndani kuunga mkono jitihada hizo.
Alisema waandishi hao kutoka China wameonyesha nia ya dhati ya
kuvitangaza vivutio vyetu na hivyo kutokana na urafiki wa kihistoria
uliopo kati ya China na Tanzania, zoezi hilo litakuwa la mafanikio
makubwa.
Aliongezea kuwa China ni nchini yenye watu wengi Dunia hivyo kupitia
waandishi hawa watakwenda kuwafikia wananchi wengi wa nchi hiyo
kupitia makala na machapisho mbalimbali kuhusiana na vivutio vya
utalii vilivyopo Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akizungumza na waandishi waandamizi wa habari kutoka China mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.
“changamoto kubwa waliyoiona ni gharama ya usafari wa ndege ni kubwa
kutokana na kutokuwepo kwa ndege za moja kwa moja,” alisema Jaji
Mihayo na kuongezea kuwa usafiri wa anga utakapo imarishwa utachochea
idadi kubwa ya watalii kutoka China.
Alisema tayari Rais Magufuli alishaahidi kuleta ndege Kubwa
itakayofanya safari ndefu hivyo itasaidia kupata soko la watalii
kutoka china kuongezeka na itasaidia kuongeza mapato katika sekta ya
utalii.
Alisema pia Halmashauri na wawekezaji katika hoteli mbalimbali
zilizopo katika maeneno ya vivutio vya utalii waunganishe nguvu ili
kutatua changamoto za barabara kwani imekuwa ni kero kwa wageni.
Miundombinu ya barabara kuelekezea maeneo ya hotel pia katika
vivutio ni mbovu hivyo Serikali kushirikiana na sekta binafsi
wajipange kuboresha miundombinu ili iwe rafiki na kuvutia watalii
zaidi alisema Jaji Mihayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akimkabidhi zawadi kwa Mhariri Msaidizi kutoka China Daily Media Group, Bw. Kang Bing(kulia) mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania. ziara hiyo iliwajumuisha wahariri sita kutoka vyombo mbalimbali vya nchini China.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Bibi Devota Mdachi alisema
ujio wa wanahabari hawa ni mwendelezo wa juhudi za TTB katika
kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ili kufanya idadi ya
watalii kuongezeka.
“ tumepokea jumla ya waandishi sita kutoka vyombo mbalimbali vya
habari vya Nchini China ikiwa ni njia mojawapo ya kuendeleza juhudi za
kutangaza vivutio vya utalii katika nchi hiyo,” alisema Bi.Mdachi
Alisema tumejipanga kukuza soko la utalii kwa kuongeza idadi ya
watilii kutoka china kwani ni moja ya nchi yenye watu wengi duniani
hivyo kwa njia ya kuwatumia waandishi wa habari itasaidia kuvitangaza
vivutio vyetu kwa urahisi zaidi.
Aliongezea kuwa pamoja na kuvitangaza vivutio vyetu ni lazima
kuboresha miundombinu hususani barabara katika maeneno ya vivutio ili
kuwapa urahisi watalii kufika katika maeneo ya hifadhi.
“Wamevutiwa sana na vivutio vyetu na wameahidi kuwa mabalozi wetu
nchini kwao wa kuvitangaza vivutio vyetu,”alisema Bi Mdachi
Alisema matumaini yetu kupitia ujio huu ni kupata watalii wengi kutoka
nchini China na njia hii ya kutumia waandishi wa habari tutaendelea
kuitumia kwa nchi nyingine ili nao wawemabalozi katika nchi zao na
hatimae kukuza sekta ya utalii nchini.
Akiongea kwa niaba ya watalii wengine Mhariri Msaidizi kutoka China
Daily Media Group Bw. Kang Bing alisema wamefurahi kuona vivutio
vilivyopo Tanzania pamoja na ukarimu wa watanzania.
“Tulitembelea maeneo mbalimbali kama Ngorongoro na ziwa Manyara na
kuona wanyama na ndege mandhari nzuri na hili limekuwa somo jipya
kwetu,” alisema Bw. Bing
Alisema tutakwenda kuwa mabalozi wa kutangaza maeneo ya vivutio vya
utalii kupitia machapisho na makala mbalimbali ili kuchochea idadi ya
watalii kutoka china kuongezeka.
Changamoto kubwa ni kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo ya
hifadhi na pia kuwekeza kwenye usafiri wa anga kwa kuwa na safari za
moja kwa moja.
Jumla ya waandishi sita kutoka Beijing Press Group, China Daily,
International Liaison Drpartment, English news service na China Radio
International walitembelea hifadhi ya Ziwa Manyara na Ngorongoro
Crater.
No comments:
Post a Comment