KUELEKEA mtanange wa kumaliza ubishi baina ya mahasimu wawili Simb ana Yanga huku kila upande ukijinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kesho kuanzia majira ya saa 11 jioni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Ni mechi ya watani wa jadi inayozungumzwa sana midomoni mwa watu, kila mmoja akijinasibu kumfunga mwenzake kwa idadi kubwa ya magoli na na kuinyakua Ngao ya Jamii.
Simba ikiwa imefanya usajili mkubwa sana na wagharama, wakiwajumuisha nyota wanne kutoka Azam Fc John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Erasto Nyoni pamoja na Kiungo Mnyarwanda kutoka Yanga aliyekipiga kwa misimu kadhaa Haruna Niyonzima.
Mbali na hao, wamemsajili golikipa wa Timu ya Taifa akitokea Mtibwa Sugar Said Dunda na Emanuel Mseja kutoka Mbao Fc, beki wa kulia Shomary Ally, beki wa kati kutoka Toto Africa Yusuf Mlipili, Salim Mbonde kutoka Mtibwa na Mshambuliaji Emanuel Okwi kutoka Sc Villa ya Nchini Uganda. Nicolaus Gyan kutoka Nchini Ghana na beki wa kushoto kutoka Mbao Jamal Mwambeleko
Kwa upande wa Yanga, wameweza kufanya usajili kwa kuwasajili Ibrahim Ajib kutoka Simba, Raphael Daud kutoka Mbeya City, Pius Buswita kutoka Mbao Fc, Gadiel Michael kutoka Azam, Papii Kabamba Tshishimbi wa Mbabane Swallows na wameweza kuwapanisha vijana wao kutoka timu B Said Musa, Maka Edward ili kuja kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wachezaji walioachwa pamoja na wale waliosajiliwa na timu zingine.
Yanga walifanikiwa kuwabakisha wachezaji muhimu kama Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe waliokuwa wamemaliza mikataba ya kuitumikia klabu hiyo ya Yanga.
Michuano hii ya Ngao ya Jamii, kwa kawaida huwa ni ‘Super Cup’, kwa maana ya kukutanisha mabingwa wa michuano miwili tofauti bingwa wa FA dhidi ya mshindi wa pili wa ligi kama bingwa wa ligi na FA.
Safari hii kuna uhalisia zaidi, watu wataona nani mkali kati ya bingwa wa ligi kuu ambaye ni Yanga na bingwa wa Kombe la FA Simba na kwa mwaka 2017 inakuwa ni mechi ya mara ya 10 toka kuanzishwa mwaka 2001, kusimama na kurudi tena mwaka 2009.
YANGA
Yanga imewezza kucheza jumla ya mechi nane ambazo ambapo katika hizo mechi 3 wamecheza dhidi ya Simba , Mtibwa ni mara 1 na Azam mara 4 aambapo ndiyo timu ambayo imecheza mechi nyingi zaidi za Ngao ya Jamii tangu ilivyoanzishwa mwaka 2001 kati ya timu nne ambazo zimewahi kucheza mechi hiyo.
SIMBA.
Simba imecheza Ngao ya Jamii mara nne ikiwa dhidi ya mahasimu wao Yanga mara (3) , Azam mara (1) na kuchukua mara 2 kisha kupotea na kuwaacha Azam wakicheza mfululizo ndani ya miaka 5 na kulinyakua mara moja msimu wa 2016/17.
Yanga imefanikiwa kuifunga Simba jumla ya mabao matano katika Ngao ya Jamii pindi ilipokutana katika miaka tofauti ambapo mwaka 2001, Wanajangwani hao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na mwaka 2010 waliifunga penalti 3-1. Lakini Simba imewafunga wapinzani wao hao jumla ya mabao manne yakiwemo mawili kwenye ushindi wa 2-0 mwaka 2011.
WAFUNGAJI SIMBA, YANGA ZILIVYOKUTANA
Yanga 2-1 Simba (2001)
Mabao ya Yanga yalifungwa na Edibily Lunyamila na Ally Yusuph ‘Tigana’ la Simba lilifungwa na Steven Mapunda.
Simba 1-3 Yanga (2010) penalti
Penalti ya Simba ilifungwa na Mohamed Banka huku Emmanuel Okwi na Uhuru Seleman wakikosa penalty, na kwa upande wa Yanga zilipigwa na Godfrey Bonny, Stephano Mwasyika na Isack Boakye.
Simba 2- 0 Yanga (2011)
Wafungaji Haruna Moshi ‘Boban na Felix Sunzu.
AZAM MECHI 5, IMECHUKUA MA R A MOJA
Azam ndiyo timu yenye historia ya kucheza Ngao ya Jamii mara nyingi zaidi na kushindwa kuchukua kombe hilo . Azam wamecheza mara tano kwenye mechi hizo na kufanikiwa kushinda mara moja pekee.
No comments:
Post a Comment