Thursday, August 17, 2017

Msipotumia Fursa Zilizopo Tanga Wageni Watazitumia-Dkt. Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongeza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akitoa neon la utangulizi wakati wa ufunguzi wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers Dkt. Jim Yonaz akielezea kuhusu malengo ya kongamano la Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.


Na Mwandishi Wetu- MAELEZO.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wakazi wa na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kuanza mapema kuzitumia fursa zilizopo katika mkoa huo kabla ya wageni hawajazitu,ia na kuwaacha wenyeji kuwa watazamaji.

Waziri Mwakyembe ametoa rai hiyo leo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano la siku moja la Fursa za Biashara ambalo lina lengo la kufungua fursa za biashara zilizopo katika mkoa na hasa katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani jijini Tanga unatarajiwa kuanza.

“Tusipojipanga leo na kuzitumia vizuri hizi fursa nyingi zilizopo basi tujue fursa hizi zitatumiwa na wageni ili hali Watanzania tunaauwezo”, alisisitiza Waziri Mwakyembe.

Alieleza kuwa kama kuna changamoto zozote zinazowakabili watu wa Tanga na Watanzania kwa ujumla katika kutumia fursa zilizopo basi ni vema Serikali ya Mkoa, wafanyabishara na wawekezaji waliopo mkoa wa Tanga wakazitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili zigeuke kuwa fursa ili Watanzania wazichangamikie.

Aidha Mwakyembe amewasisitiza Watanzania kuwekeza katika biashara ya huduma na viwanda vya uzalishaji bidhaana bidha ambapo vitakuwa vikihudumia ujenzi wa miradi mbalimbali hususani bomba la mafuta kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanga, Tanzania.

Ameeleza kuwa hivi sasa kasi ya wageni kutaka kutumia fursa za bomba la mafuta imekuwa kubwa ambapo ameeleza kuwa kuna baadahi ya wafanyabiashara kutoka nchi jirani wamekuwa wakifanya ushawishi ili wafanyakazi na wataalamu watakaokuwa katika mradi wa bomba la mafuta wawe wanatumia huduma za hoteli za nchi hiyo.

Akiongea awali, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alieleza kuwa wananchi wa Mkoa wa Tanga wameendelea kujipanga kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa zilizopo Tanga kwa ajili ya kukukuza kipato na uchumi wa mkoa wa Tanga.

“Tumejiandaa vya kutosha na wakati ni sasa na hatuna sabababu za kuchelewa kutumia fursa zilizopo”, alieleza Mkuu wa Mkoa huku akitaja baadhi ya uwekezaji unaotarajiwa kufanywa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya cha Saruji, ujenzi wa hoteli, kilimo, upanuzi wa uwanja wa ndege na uimarishaji wa miundombinu ya reli na bandari.

Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Dkt. Jim Yonaz aliwataka wananchi na wafanyabiashara wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa wanakuwa na haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa za ukuaji wa uchumi wa mkoa ili wawe sehemu ya fahari ya kuirudisha Tanga ya viwanda kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Dkt. Yonaz alieleza kuwa kuwa TSN wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inashirikiana na Serikali ya mkoa kwa kutoa elimu kupitia magazeti ya Daily News na HabariLeo kutangaza fursa mbalimbali zilizopo mchini ili wananchi waweze kuzifahamu na kuzifanyia kazi.

Jukwaa la Fursa za Kibiashara linaloandaliwa TSN ni la kwanza kufanyika katika mkoa wa Tanga na la tatu kufanyika hapa nchini ambapo la Jukwaa la kwanza lilifanyika mkani Simiyu na lile la pili lilifanya mkoa wa Mwanza. Aidha kwa mujibu wa waandaji, jukwaa kama hili linatarajiwa kufanyika hivi karibuni Visiwani Zanzibar na baadae katika mkoa wa Arusha.

No comments: