Tuesday, August 22, 2017

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELA MIRADI YA UMEME WA GESI YA KINYEREZI II NA ULE WA UPANUZI KINYEREZI I

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (Mb), wapili kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, kutembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2018. Kamati hiyo pia ilitembelea kituo cha kupkea gesi asili kilicho jirani na Miradi hiyo.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imetembelea miradi ya kuzalisha umeme wa gesi ya Kinyerezi II, na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I unaoendeshwa na Serikali kupitia Shrika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, pia ilitembelea kituo cha kupokea gesi asili inayotumika kuzalisha umeme kilichoko jirani na miradi hiyo.
Katika ziara hiyo, mwenyeji wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Mb), Mhe.Dkt.Medard Kalemani, aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miradi hiyo inaendelea kama ambavyo Serikali ilitarajia na kwamba Watanzania wategemee ongezeko kubwa la upatikanaji wa umeme pindi miradi hiyo itakapokamilika. “Mhe. Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati, miradi hii kunzia ule wa Kinyerezi I unaopanuliwa ambapo kutakuwa na ongezeko la umeme Megawati 35 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 185 zitakazozalishwa kutoka Kinyerezi I, na huu wa Kinyerezi II utakapokamilika Agosti mwakani (2018) utatupatia Megawati 240 na ukijumlisha na miradi mingine itakayofuatia ya Kinyerezi III na VI, tutakuwa na jumla ya Megawati 1175.” Alifafanua Mhe. Dkt. Kalemani.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephene Manda aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya mashine 8 ambazo zitafua umeme na tayari ufungaji wa mashine hizo umeanza na unaendelea na kuongeza kuwa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, TANESCO itaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na kufanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kadri kazi ya ufungaji wa mashine hizo utakavyokuwa unakamilika.
Alisema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

Wajumbe wa Kamati hiyo pian walipata fursa yua kujionea kazi ya utandazaji wa mabomba makubwa ya kupitisha gesi kutoka kituo cha kupkea gesi kuelekea kwenye eneo la miradi hiyo.



“Niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na haya ndio matarajio ya wabunge kuona kuwa miradi hii ambayo inagharimu fedha nyingi za walipa kodi inakamilika kwa wakati ili hatimaye serikali iweze kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kama ilivyoahidi wananchi.”Alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia. Baada ya kumaliza ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi hiyo ya umeme wa gesi asilia.


 Dkt. Kalemani (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe hao baada ya kutembelea eneo la mradi wa upanuzi Kinyerezi I
 Hili ndio eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi II
 Mtandao wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia kutoka kituo cha kupokea gesi hiyo kuelekea eneo la miradi hiyo.
 Mafundi wa TPDC wakiwa wamesimama kwenye eneo la utandazaji wa mabomba hayo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia, (wapili kushoto), akizungumza jambo wakati akiongozana na Naibu Waziri Dkt. Kalemani (kushoto) na wajumbe wa kamati.
 Mhe. Hawa Ghasia akiwa tayari kuanza ziara.
 Dkt. Kalemani akiongea wakati wa ziara hiyo.
Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, wakati wajumbe wa Kamati walipowasili eneo la Miradi.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC), Mhandisi  Kapuulya Musomba(kulia), akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania, (TANSCO), Dkt. Alex Kyaruzi, (katikati), na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Dkt. James M. Nzagi.
  Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James


 Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O. Ikwasa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania, (TANSCO), Dkt. Alex Kyaruzi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (wakwanza kulia) na  Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James wakiwasili eneo la mradi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwaonyesha kitu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo, (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Jerome Dismas Bwanausi




 Mhe. Hawa Ghasia akizungumza baada ya ziara ya kutembelea kituo cha kupokea gesi asilia kinachosimamiwa na TPDC.
 Wajumbe wa Kamati wakipita pembezoni mwa moja ya mashine kubwa (genereta), kati ya 8 zinazofungwa kwenye mradi wa Kinyerezi II
Mhandisi Manda, (waliyenyoosha mkono), ambaye ni Meneja Mradi wa Kinyerezi II, akwapatia maelezo wajumbe wa Kamati akiwemo Naibu Waziri Dkt. Kalemani.

No comments: