Thursday, August 10, 2017

JK NA LOWASSA WAJUMUIKA NA MAMIA YA WANANCHI MAZISHI YA BILIONEA MREMA ARUSHA

 Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilionea marehemu Maleu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika jana katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha(Habari Picha NA Pamela Mollel,Arusha)
Waziri Mkuu mstaafu,Edward  Lowassa akiweka shada la maua pamoja na mke wake  katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema jana nje kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha
 Baadhi ya wake za marehemu wakiweka udongo katika kaburi la mpendwa wao

 Waziri Mstaafu wa mambo ya nje Benard Membe akiweka shada la maua katika kaburi la Bilione Mrema

 Meneja mahusiano Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)Pascal Shelutete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilione Mrema.
 Watoto wa marehemu wakiwa wamebeba mashada ya maua

 Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete wakisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu,Edward  Lowassa katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema leo nje kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
 Baadhi ya wanakamati wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mrema kuelekea katika eneo maalumu lililotengwa na familia kwaajili ya maziko
 Hapa watoto wakiwa wanaweka udongo katika kaburi la baba yao
 Wake wa marehemu wakiwa wanaingia katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya maziko
 Kulia ni Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete,katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na
Abdulrahman Omari Kinana wakiteta jambo katika msiba wa Mrema
 Wake wa marehemu Mrema wakiwa katika huzuni kulia aliyevalia suti nyeusi ni baba mzazi wa Bilionea huyo
 Mh Abdulrahman Omari Kinana mara baada ya kuweka shada la maua
 Jeneza la marehe Bilionea Maleu Mrema likiwa linashushwa katika nyumba yake ya milele

Wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete
Nyumba ya milele ya Bilionea Maleu Mrema 

No comments: