Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (katikati) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman
Mbowe ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti,
mara baada ya kuwasili katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae
(tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga kwa ajili ya kuanza
ziara hiyo
Msimamizi
wa Uzalishaji na Ujenzi katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha
Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Said Ngongoki
akielezea jinsi uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo kwa Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
(katikati) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara
walipofanya ziara kiwandani hapo
Meneja
Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha
Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa ( wa
kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Bajeti katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (katikati) akibadilishana mawazo na mwakilishi kutoka Idara ya
Biashara katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill
Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Emily Wu (kulia) katika eneo la
uzalishaji la kiwanda hicho.
Mtaalam
kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Dominick Ngunyali
(kulia) akitoa ufafanuzi juu ya jinsi gesi inavyopokelewa katika
Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo
Mkuranga mkoani Pwani kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti
katika eneo la kupokelea gesi hiyo
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (mbele kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Bajeti kwenye ziara katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae
(tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Meneja
Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha
Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa (kushoto)
akielezea jinsi udongo wa aina mbalimbali unavyochanganywa katika hatua
za awali za maandalizi ya utengenezaji wa vigae (tiles) kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (kulia) akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Mitambo katika Kituo
za Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi cha Somangafungu kilichopo mkoani
Lindi, Edwin Konyani katika ziara hiyo.
Msimamizi
wa Bomba la Gesi Upande wa Umeme katika Kituo cha Kupokea Gesi kutoka
Songosongo na Madimba Joseph Msafiri (katikati) akielezea jinsi gesi inavyopokelewa katika kituo hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika ziara hiyo.
Sehemu ya Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba kilichopo Somangafungu mkoani Lindi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo ameongoza Kamati y Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika maeneo
mbalimbali yenye miradi ya gesi katika mkoa wa Lindi lengo likiwa ni
kuona utekelezaji wa miradi hiyo.
Kati ya maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Somangafungu, Makutano ya Bomba la Gesi Asilia (Somangafungu) mkoani Lindi pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa Mitambo ya Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) lililoko katika Manispaa ya Lindi.

No comments:
Post a Comment