Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani amefanya kikao cha kazi na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati
na Madini pamoja na Taasisi ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme la Tanzania
(TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti
na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta
kwa Pamoja (PBPA), Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST) Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Lengo
la kikao hicho lilikuwa ni kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa
Wizara.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na
watendaji pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake
(hawapo pichani) katika kikao hicho. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na kushoto ni
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe (kushoto)
akielezea mafanikio ya sekta za nishati na madini nchini katika kikao hicho.
Sehemu ya watendaji na wafanyakazi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi
zake wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Haji
Janabi akitoa mchango wake kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi kutoka Idara ya Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini, Amon MacAchayo
akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Philip Mathayo
akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mjiolojia kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Ezekiel Seni akitoa
maoni yake katika kikao hicho.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Joseph Mtui akielezea mikakati ya
uboreshaji wa chuo hicho katika kikao hicho.
No comments:
Post a Comment