Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
UZALISHAJI
wa Maji Safi kunahitaji kuwepo na miundombinu ya maji taka ambayo
yanazalishwa na maji safi katika kutunza mazingira pamoja na afya kwa
wananchi wanatumia maji safi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu
wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, Mhandisi Romanus
Mwang’ingo amesema kuwa wameanza kufanya utekelezaji wa miradi ya
ukusaji na uondoshaji wa majitaka kwa kuanzisha miradi mitatu ya kisasa
ya kusafisha majitaka hayo.
Amesema
Miradi hiyo itakwenda sambasamba na uzalishaji wa mabomba ya kukusanya
majitaka hayo kwa kujenga miundombinu katika maeneo ya Jangwani, Mbezi
Beach pamoja na Kurasini.
Mwandisi
Mwang’ingo amesema ujenzi wa miundombinu hiyo itaongeza kiwango cha
kusafisha majitaka kwa asilimia 30 ifikapo 2020 kutoka kiwango cha
asilimia 10 iliyopo sasa itakayogharimu Dola za Kimarekani Milioni 600
katika mwaka wa fedha 2017/2018.
Amesema
mfumo wa majitaka wa Jangwani utakapokamilika utakuwa na uwezo wa
kusafisha majitaka hayo mita za ujazo 200,000 kwa siku.
Mabomba
yenye urefu wa kilomita 376 yatajengwa katika mradi utakaonzia kunazia
Ubungo hadi Jangwani,Kinondoni, Mwananyamala, Msasani Katikati ya Jiji
na Ilala.
Mhandisi
Mwang’ingo amesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha sehemu
sehemu itakayoweza kusafisha mita za ujazo 25,000 kwa siku na mabomba
yenye urefu wa kilomita 17.43 yatakayojengwa eneo la magomeni.
Aidha
katika awamu ya kwanza,bomba linalomwaga majitaka baharini litaacha
kutumika na badala yake majitaka hayo yatakwenda kusafishiwa katika
mtambo huo ambapo mtambo huu unajengwa kati ya ushirikiano wa Serikali
ya Tanzania na Serikali ya Korea kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka
Benki ya Exim ya Korea unaotarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani milioni
90 ambazo tayari zimepatikana.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam,
Mhandisi Romanus Mwang’ingo (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari juu ya mikakati Dawasa ya maji safi na majitaka leo jijini Dar es
Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maelezo,Rodney Thadeus
kulia ni Meneja Mawasiliano Dawasa, Neli Msuya.
Meneja
wa Mawasiliano wa Dawasa, Neli Msuya akizungumza juu miradi inajengwa
na Dawasa katika maeneo mbalimbali Dar es Salaam na Sehemu ya mkoa wa
Pwani leo jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment