
Siku ya jana Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) chenye kaulimbiu ya Dira ya Mabadiliko kimetimiza miaka mitano tangu kupata usajili rasmi 22 Agosti 2012.
Mwenyekiti Hamad Rashid ameuzungumzia mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha CUF na kueleza kuwa hatua waliyofikia ya kupelekana mahakami siyo sahihi kwani itazidi kuchochea mgogoro huo.
Hamad Rashid amefafanua kuwa ADC ilikuwa na mgogoro na aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho Said Miraji na wenzake wanne lakini wameumaliza mgogoro wao kwa majadiliano bila kufikishana mahakamani, hivyo ni vyema CUF wakaiga mfano huo na kuziondoa tofauti zao.
Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo ameeleza kuwa zuio la kufanya mikutano ya kisiasa limekwamisha utendaji kazi wa ADC kama chama kinachohitaji kujitangaza kwa wananchi.
Vilevile Katibu Mkuu Doyo amesisitiza kuwa Chama chao kitaendelea kupinga vikali kuwatumia vijana katika kufanya vurugu na maandamano yasiyo na tija, ndoa za jinsia moja, na adhabu ya kifo.
No comments:
Post a Comment