Lengo ni kuwafikia waliowengi na huduma za kibenki kwawasio na akaunti za benki.
Dar
es Salaam Tanzania, Jumatatu 14 Agosti 2017 – Ikiwa ni moja kati ya
mikakati yake ya kuendelea kuboresha huduma zake kwa kutoa huduma kwa
kila mtanzamia hasa kwa wale wasio na akaunti za Benki, Benki ABC
Tanzania leo imezindua huduma za wakala itakayowawezesha wateja wake
kupata huduma za kibenki hiyo wakiwa katika mazingira yeyote yale.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha
Wateja binafsi Bi.Joyce Malai alisema Benki ABC inaendelea kuja na
teknolojia mpya katika utoaji huduma ili kukidhi mahitaji ya kibenki kwa
wateja wake nchini Tanzania.
Changamoto
ya Kipato kidogo na kuhitajika kwa vielelezo vingi wakati wa kufungua
akaunti za Benki pamoja na uhaba wa huduma za kibenki kwenye baadhi ya
maeneo hapa nchini yamefanya Watanzania wakose huduma za kibenki na
hivyo kufanya maendeleo ya kiuchumu ya nchi kuwa finyu. Sisi Benki ABC
tumejiandaa kuhakikisha kwamba huduma za uwakala za Benki yetu zinakuwa
ni suluhisho kwa Watanzania kupata huduma bora za kifedha wakiwa popote
bila ya kupata shida, alisema Joyce.
Aliongeza
kuwa kama Benki inayokua kwa kasi hapa nchini, benki ABC inalengo
kupanua huduma na uwepo wake kwenye miji mikubwa hivyo huduma za uwakala
zitakuwa ni moja ya njia ya kufikia malengo hayo.
Joyce
aliongeza kuwa huduma za uwakala za Benki ABC itakuwa na tija kwa
Watanzania ambao hawana akaunti za Benki na pia kwa wale ambao wana
akaunti lakini badala ya kupoteza muda mwingi kupanga foleni kwenye
matawi yao wanaweza kupata huduma hizo kwenye wakala wa Benki hiyo
popote pale. Huduma za wakala zitaanza kupatikana jijini Dar es Salaam
kupitia Maxcom Afrika. Wateja wa Benki ABC watapata huduma zote za
kibenki kupitia wakala wote wa Maxmalipo kwa mkoa wa Dar es Salaam kabla
ya huduma hiyo kusambaa nchini kote.
Mkuu
huyo wa Kitengo cha Wateja binafsi alisema wakala wa Benki ABC watatoa
huduma za kibenki zikiwemo kufanya miamala mbali mbali ambazo hapo awali
ziliwalazimu wateja kupanga foleni kwenye matawi ya Benki hiyo zikiwemo
kuweka na kutoa fedha, kulipia ankara mbalimbali kama maji, umeme,
huduma za kufungua akaunti na kupata au kubadilisha kadi ya Benki.
Huduma hizi pamoja na nyinginezo zitapatikana kwa wateja wa Benki ABC
kupitia Maxmalipo.
Joyce,
aliwahakikishia wateja wa Benki ABC kuendelea kuwa tayari kupata huduma
nyingine nyingi zenye tija na manufaa kwa ajili yao. ‘Tutaendelea
kuwekeza zaidi kwenye huduma zilizo bora zaidi na kwa kuanza wateja wetu
wanaweza kujidhihirishia jinsi huduma za uwakala zitakavyokuwa na tija
kwao kwa kurahishisha huduma za kibenki pamoja na kuokoa gharama na muda
wa kupanga foleni na kutembea umbali mrefu ili tu kupata huduma za
kibenki.
Tumeungana
na Maxcom Afrika Plc ambao wana mawakala wengi hapa nchini Tanzania na
hivyo tunaamini tutafanikiwa sana kufikia wateja wengi na kufanikisha
lengo letu, aliongeza Joyce.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Afrika Plc Jameson Kassati
alisema kwa sasa mawakala wa Maxmalipo wanafanya miamala zaidi ya
700,000 kwa siku. ‘Tunajisikia fahari sana kushirikiana na Benki ABC
ambayo kwa mwaka huu imeshinda tuzo ya kuwa Benki bora na inayokuwa hapa
nchini Tanzania, Maxcom Afrika Plc ndio yenye wakala wengi nchini
Tanzania ambapo kwa sasa kuna jumla ya wakala 16,000. Maxcom ndio
ilikuwa ya kwanza kuzindua huduma za uwakala wa kibenki hapa nchini.
Maxmalipo inatumia teknolojia ya utaalamu wa hali ya juu ambapo tumeweza
kufanikisha kurahisisha Malipo mbali mbali kwa uharaka zaidi ikiwemo
ile ya Malipo ya maji, umeme na mengineyo.
Akiongea
kwenye hafla hiyo, meneja wa huduma za uwakala Benki ya ABC Mwita Robi
alisema, ‘kwa hapa tulipofikia, matawi ya Benki ABC yatakuwa na umuhimu
mkubwa kwani huduma zote za uwakala zitaunganisha na matawi hayo kwa
ajili ya kuhakikisha viwango vya huduma zote zakibenki zinapatikana na
kuzingatia taratibu zote za utoaji wa huduma za kibenki.
Huduma
ya hii ya uwakala kwa mabenki inatolewa duniani kote na inatajwa kuwa
moja ya njia rahisi na nyepesi ya kuwafikia wateja wengi hasa wasio na
akaunti za Benki, aliongeza Mwita.
Benki
ABC ambayo ni moja ya kampuni tanzu za Atlas Mara, ilishinda tuzo ya
kuwa Benki bora Afrika kwa mwaka 2017 ambapo bado imeendelea kujidhatiti
na kuenea zaidi hapa nchini kwa kufungua matawi mengi zaidi ambapo
mwaka huu pia imejipanga kuzindua matawi mawili katika mkoa wa Dodoma na
Mwanza.
Meneja wa Kitengo Binafsi Benki ya ABC Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari wa uzinduzi wa huduma za uwakala wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Maxcom Africa Plc.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Africa Plc Jameson Kasati akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari jana kwenye hafla ya kushirikiana na Maxcom Africa Plc kutoa huduma za kibenki.
Meneja huduma za uwakala wa Benki ABC Mwita Robi akionyesha mashine ya uwakala wa huduma za kibenki jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuzindua huduma za hiyo jana.
No comments:
Post a Comment