Wednesday, July 12, 2017

WAZIRI WA ZANZIBAR KUFUNGA MAONESHO YA 41 YA BIASHARA KIMATAIFA KESHO

Na Chalila Kibuda, Global ya Jamii

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum anaratajiwa kuwa mgeni rasimi kesho katika ufungaji wa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade) ilisema kuwa maonesho hayo yataitimishwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum ambaye atatoa vyeti kwa washindi wa mabanda bora yaliyoshiriki maonesho hayo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa maonesho hayo yatafungwa majira ya saa saba kwa hotoba ya Waziri huyo na kufuatana na viongozi mbalimbali wakiwemo waandaji wa Maonesho hayo.

Wakati huo katika maonesho hayo wananchi wameendelea kufika katika viwanja vya sabasaba kwa kupata huduma pamoja bidhaa za washiriki.

Mabanda ambayo yamekuwa na watu katika siku ya maonesho tangu siku kwanza hadi leo ni mabanda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Profesa Adolf Mkenda akimpa maelekezo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ,Mcharo Mrutu katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Profesa Adolf Mkenda akisaini kitabu cha wageni katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akipata huduma katika banda Chuo cha Taifa Usafrishaji (NIT) katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata huduma katika banda la Wakala Usajili , Ufilisi na Udhamini (RITA) katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa maonesho ya ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments: