Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake mbele ya maafisa wa
Magereza pamoja na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, katika Ukumbi
wa Magereza Karanga, Mjini Kilimanjaro Mkoani Kilimanjaro, Julai 14,
2017. Waziri Mhagama alifanya ziara ya kutembelea na kukagua eneo la
Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha karanga kilichopo
mkoni Kilimanjaro ambacho kipo chini ya Mfuko wa Pesheni wa PPF kwa
kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini. Kiwanda hicho kilikuwa
kinazalisha viatu 150 kwa siku na sasa kinatarajiwa kufikia viatu 400
baada ya kukamilika kwa ukarabati.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni,
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira, Katibu mkuu Wizara ya Viwanda
Biashara na Uwekezaji, Prof. Adof Mkenda pamoja na Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt, Juma Malewa wakiangalia sehemu ya Bidhaa za Ngozi
zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani
Kilimanjaro, Julai 14, 2017.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama, akichukuliwa kipimo cha mguu kwa ajili ya
kutengenezewa Viatu vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha
Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
wakiangalia moja ya mashine za kutengeneza viatu, katika Kiwanda cha
Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. Wengine
ni Kamishna wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Hassan Bakari Mkwiche
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akitoa taarifa fupi ya
uwekezaji uliofanywa na mfuko huo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza
katika ukarabati wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Magereza Karanga
kilichopo Mkoni Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment