Friday, July 28, 2017

WANAHABARI WAHAMASISHWA KUANDIKA HABARI ZA KUUTANGAZA UTALII WETU

Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. .

Akiwasilisha mada ya Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini,Dkt Abbas alisema kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wana wajibu wa kuwashirikisha Wanahabari kwa kuwapatia taarifa sahihi,Ili jamii nayo ielimishwe habari zenye usahii.

"Tuwafadhili Waandishi wa habari kufanya stadi muhimu kama habari za Takwimu (data Journalism) na za uchunguzi (investigative journalism) kwa habari zenye maslahi kwa Taifa kama vile kufichua mitandao ya Waharifu wa mazingira au Majangili",alisema Dkt Abbas.

Dkt.Abbas amewataka Wanahabari kuandika habari za Utalii kwa wingi katika suala zima la kuutangaza Utalii wa nchi yetu,ambao ukitangazwa vizuri itasaidia kukuza uchumi wetu na hatimae kuongeza pato la Taifa,akaongeza kuwa pia na jamii inayozunguka katika suala zima la utalii itanufaika kwa namna moja ama nyingine.
Pichani kati ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Dkt Ayub Rioba akiwa sambamba na Meneja Mahusiano wa TANAPA,Pascal Shelutete na wadau wengine wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas alipokuwa akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil  Makunga  akiwa na Wajumbe wengine katika Mkutano wa Wahariri na Waandishi waandamizi  ulioandaliwa na Tanapa
Wahariri na Waandishi waandamizi wa Habari walioshiriki katika Mkutano Maalum wa Mwaka ulioandaliwa TANAPA juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda 
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mkoa wa Morogoro Lilian Lucas  akipitia jarida la Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro wakati wakati somo la umuhimu wa kuhifadhi na kutangaza utalii wa eneo hilo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda  akichangia jambo kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini, wakati wa mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil  Makunga  akiuliza moja ya swali kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini,katika mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.

No comments: