Monday, July 10, 2017

WAKUU WA SHULE BINAFSI WALIPE BIMA ZA AFYA KWA WANAFUNZI –SPIKA MSTAAFU MAKINDA

 .Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akikabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto chini ya miaka 18 kwa wanachama wapya katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, ,Anne Makinda amesema wakuu wa shule binafsi wanachukua  fedha za huduma ya matibabu ya afya kwa wanafunzi lakini wanafunzi hao wamekuwa hawapati  huduma wanazostahili na kulingana na kiasi walicholipia.

Wakuu wa Shule binafsi wamekuwa wakilipisha wanafunzi fedha za huduma ya matibabu ikiwa ni njia moja ya maelezo kujiunga (joining instruction) ila inapotokea mtoto anaumwa humrudisha kwa wazazi wake.

Mwenyekiti huyo ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la NHIF katika Maonesho ya biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, amesema mwanafunzi akilipia bima ya afya lazima atumie na sio kubaki mzigo kwa mzazi wakati alishalipia fedha ya matibabu hiyo.

Amesema kuwa wakuu wa shule wanatakiwa kujiunga na  mfuko wa taifa ya wa bima ya Afya NHIF ili kuweza kuwahudumia wanafunzi katika kupata matibabu.

Anne Makinda amesema kuwa katika maonesho ya sabasaba wamesajili bima za afya kwa watoto 1600 na kuongeza kuwa wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kupata bima za afya.

Amesema kuwa wameboresha bima ya afya katika mfuko wa afya ya jamii katika halmashari kwa kila aliyepata bima kutibiwa mkoa mzima tofauti na hapo nyuma kutibiwa katika Wilaya husika.

Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa huduma za bima za afya ikiwa ni pamoja na serikali kuweka mpango wa kila mtu kuwa na bima ya afya.


.Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, , Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti , Angela Mziray katika banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Wanachama wa NHIF, Ellentruda Mbogoro katika banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Sheik Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akipata maelezo kutoka kwa Meneja Wanachama wa NHIF, Ellentruda Mbogoro katika banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Rose Mdami wakati alipotembelea banda la NIDA katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi , Sebera Fulgence katika banda la Mfuko huokatika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments: